Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BAIM-R8LS1m.jpg
 
Mshambuliaji mahiri na nahodha wa Barcelona, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya jana Jumanne kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.

Mabao hayo aliyafunga katika mechi ya kwanza ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, yamemfanya Messi raia wa Argentina kuwa mchezaji anayeongoza barani Ulaya kwa kufunga 'hat trick' nyingi zaidi ya wengine.

Mchezaji huyo alianza kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa faulo ‘free-kick’ dakika ya 31, ikiwa ni faulo ya nane kwake kufunga kwa mwaka 2018, kabla ya kukamilisha 'hat-trick' ya 42, kwa Barcelona dakika za 77 na 87, ikiwa ni ya nane kwake kwenye michuano ya Ulaya, sita alizifunga kwenye timu ya Taifa ya Argentina.

Aidha Messi ameweza kuifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Raul kwa kufunga mabao 104 katika michuano ya Ulaya akiwa ameyafunga katika michuano 14 tofauti.
King messi hana mpinzani
 
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amemfagilia mshambuliaji wake Daniel Sturridge, akisema tangu amemfahamu hajawahi kumwona

akicheza kwa kiwango cha juu kama alivyofanya juzi dhidi ya PSG ya Ufaransa.

Liverpool iliikaribisha PSG na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, Sturridge ndiye aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 30 na James Milner akaongeza la pili dakika ya 36 kabla ya mtokea

benchi Roberto Firmino kuipa ushindi dakika ya 90.

Klopp alisema, PSG iliwawekea ulinzi wa kutosha Sadio Mane na Mohammed Salah na kuwapuuza wengine akiwemo Sturridge

aliyewadhibu kabla Firmino, aliyeingia badala yake kuihakikishia Liverpool ushindi.
This is anflied, This is What they do!!
 
Back
Top Bottom