Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

“Kamera ina athari kubwa sana katika maisha yetu. Inaweza kuharibu taswira ya mtu mbele ya jamii, na inaweza kuharibu maisha ya mtu hali kadhalika. Wasanii wakubwa duniani hawatoki ndani bila ya kuwa nadhifu au bila ya kujipodoa. Kwa nini? Kwa sababu ya wasanii wao wa vipodozi. Wasanii wao wa vipodozi hawataki waajiri wao wawe na taswira mbaya mbele ya wateja wao ambayo ni jamii. Kuwa na taswira mbaya mbele ya jamii kunaweza kusababisha wao (wasanii wa vipodozi) pamoja na waajiri wao, wasiishi vizuri hapa duniani kama wanavyotaka. Kioo ni kitu au mtu. Kama huna uwezo wa kumiliki vipodozi, miliki kioo. Kama huna uwezo wa kumiliki kioo, miliki rafiki. Kioo (hasa kitu) hakina unafiki. Usitoke ndani bila kuridhika na taswira yako.”
 
BjC4DgYhWd9.jpg
 
Mungu alikupa maisha akakupa akili ili utambue jema na baya na akakupa amri zake ili uishi kwa amani na upendo. Kama Mungu hayupo mwanamume na mwanamke walitoka wapi? Wazazi wako walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi?”
 
“Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.”
 
“Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.”
 
“Siri ya utajiri ni mawazo ya mtu. Maisha unayoishi uliyataka mwenyewe. Amka uishi. Hii ndiyo siri kubwa ya utajiri kuliko zote ulimwenguni. Ukifikiria chanya maisha yako yatakuwa chanya, ukifikiria hasi maisha yako yatakuwa hasi. Unachofikiria ndicho unachokuwa. Siri ya mafanikio yako ni jumla ya mambo unayoyawaza.”
 
Siri ya mafanikio yako ni chumba chako. Dali linasema anga ndicho kipimo cha kufikiria; Dirisha linasema utazame nje uone fursa zilizopo ulimwenguni; Feni linasema uwe mtulivu usikurupuke kufanya lolote; Kalenda inasema uwe mtu anayekwenda na wakati; Kioo kinasema ujitazame na ujiamini kabla ya kutenda lolote; Kitabu cha dini kinasema unapaswa kumwamini Mungu ili uishi; Kitanda kinasema ujifunze kuwa na likizo; Mlango unasema usipitwe na fursa ya aina yoyote ile hapa duniani; Saa inasema kila sekunde ina thamani sana katika maisha yako hivyo tumia muda wako vizuri. Amka uishi.”
 
  1. “Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo.
  2. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.
  3. Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.
  4. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.
  5. Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.
  6. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.
  7. Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.
  8. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.
  9. Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.
  10. Maskini ana woga. Tajiri hana woga. Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha.
  11. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi.
  12. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi. Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa.
  13. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.
  14. Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.
  15. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.
  16. Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.”
Leo mkuu umeamka vizuri. Yaani unashusha nondo za kufa mtu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom