Walikuwa kwenye starehe wanakunywa pombe ndipo mwanaume akachepuka kichakani na mwanamke mwingine ndipo mkewe akamfuata kisha kumchoma kisu na kumjeruhi mwanamke aliyekuwa naye," amesema Kiberiti.
Mwenyekiti huyo amewashauri wananchi kulinda na kuthamini ndoa na familia zao kwa kuepuka kujichukulia sheria mkononi na inapotokea basi wapeleke mashauir yao kwenye mamlaka husika.
Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kasenyi inayomilikiwa na Kanisa la ELCT, Dk Martin Lujimya amesema majeruhi aliyejeruhiwa mkono wa kushoto ameshonwa majeraha yake na anaendelea na matibabu.