iii/ Kupotea - kushindwa kutoa matunda yoyote; pale walipotishika na bahari iliyochafuka na
kutishika kuangamia Yesu aliwauliza imani yenu iko wapi?? kwa maneno mengine
mmeipotezea wapi?
(Luka 8: 23) Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. 24 Wakamwendea,
wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka,
akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. 25 Akawaambia, Imani
yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata
anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?