Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipindi cha mpito.
20181001_220114.jpg
 
V. Kubwa - Inasababisha mambo makubwa; imani kama ya yule akida aliyemwambia Yesu
sema Neno tu na mtumishi wangu atapona (Math. 8: 5-11).
Pasipo imani hauwezi kumpendeza Mungu (Ebr. 11: 6). Ni vizuri imani yako ikue ili uweze
kutumika vema na kuyatenda mapenzi ya Baba Mungu.
Tabia za imani nne za hapo juu
zinawakilisha uchanga wa imani na kukosa kuwajibika kwa Mkristo aliyetegemewa kusimama
katika imani. Imani huja kwa kusikia neno la Kristo (Rum 10: 17) na katika kuendelea kukaa
katika wokovu na kuikulia imani, miujiza mingi hupatikana na ujuzi katika kutembea na Mungu.
Mfano mzuri kuhusu kukua katika imani ni jinsi mtoto mdogo anapokuwa bado hajakua katika
kimo (urefu) fulani haweza kufikia vitu vilivyowekwa juu ya meza au hata kufungua vitasa vya
milango lakini kadiri anapoendelea kukua inafikia kipindi anavifikia vitu vya juu bila shida
yoyote. Mtoto huyo atakapojilazimisha kujinyoosha kwa nguvu zote ili ashike vitu vya juu kabla ya kukua ana hatari ya kujiumiza. Jambo hili ndilo linalotokea wakati ambapo mtu yoyote anapojaribu kulazimisha kutembea katika kiwango cha imani ambacho hajakifikia. anaweza akakatishwa tamaa kwa kunia mambo makubwa sana zaidi ya ilivyompasa kunia kulingana na
kimo cha imani aliyonayo. Yesu aliongezeka kimo na alipofika umri fulani (kwenye miaka 30)
alianza kutenda kazi alizokusudiwa na Mungu azitende.
Wakati fulani wanafunzi wa Yesu walikuwa wakiogopa sana na kushindwa kusimama katika
imani ipasavyo lakini imani zao zilipokua, ishara na miujiza zilianza kufuatana nao na kutenda
mambo makuu ya imani. Yesu alimwambia Petro uwa nimekuombea wewe ili imani yako
isitindike na utakapoongola uwa imarishe wenzio (Lk 22: 31-32).
 
Back
Top Bottom