Anaandika *Profesa Anna Tibaijuka*
Nijuavyo mimi Mhe Rais wetu Magufuli ni mcheshi sana. Huwa anapenda kutania lakini wengine labda tunamiss huo utani. Sasa hizi habari ati kasema kuna uwezekano wa kila mwanaume mtanzania kuoa wanawake wawili wawili ati kwa kuwa ni wengi kwa nini magazeti yetu kama Nipashe yanauchukulia literally kama ni kweli kasema hivyo?
Niko Marekani sijaona hiyo audio clip ya Rais ila naona anakuwa quoted out of context. Kiuhalisia haiwezekani kuwa na wanawake wawili wawili. Hakuna wanawake wengi namna hiyo. Kwa kuzaliwa ni hamsini kwa hamsini. Tofauti ni ndogo tunasema "it is not statisticall significant". Mungu anabalansi jinsia zote.
Sensa ya mwisho ni ya mwaka 2012. Ilibaini kwamba Tanzania ilikuwa na watu milioni 44,928,923. Kati ya hao wanaume walikuwa 21,869,990. Wanawake 23,058,933. Ongezeko kila mwaka asilimia 2.7%. Kwa hiyo mwaka 2018 Tanzania inakadiriwa kuwa na wanaume 23,066,912 na wanawake 27,786,401. Jumla 50,853,314.
Je kuna wanawake wangapi kwa kila mwanaume kwa sasa? Unachukua milioni 27 unagawa kwa milioni 23 unapata 1.204.... kwa hiyo hakuna uwezekano wa kila mwanaume kuoa wake wawili wakatosha!
Kwa maneno mengine sera ya wake wawili wawili haitekelezeki kwani hakuna wanawake wa kutosha. Namba hazikubali.
Sasa hiki kinachoongelewa cha wanawake kuonekana ni wengi kuliko wanaume tunakielezeaje??
Ni sababu za kijamii na kiuchumi wanaume wana hali ngumu zaidi kuliko wanawake. (They have a higher propensity to fall out socially). Wanaume wengi wamefungwa wamelowea wanatumia madawa ya kulevya hawana kazi huku jamii ikiwataka wanawake kuolewa na mtu mwenye uwezo. Kwa hiyo ni wanaume Wanasakamwa zaidi na tatizo la umaskini. Wanaume wengi wanashindwa kumudu familia na kuzitunza kwa hiyo ama hawaoi au wanatelekeza familia zao. Kwa hiyo ukiangalia unakuta wanaume wapo lakini wengi hawana uwezo wa kuoa wazungu wanasema siyo "eligible bachelors".
Kwa hiyo mimi ninashauri tuwasaidie wanaume na kuwawezesha kuwa "eligible bachelors".
Anayetaka utafiti zaidi soma publication yangu ya kwenye jarida maarufu la Journal of World Development Vol 25 No 6. Publishef by Pergamon Press of the American University in June 1997. "AIDS and Economic Welfare in Peasant Agriculture: Case Studies from Kagabiro Village, Kagera Region, Tanzania".
Ninayaongelea kwa kirefu zaidi. Polygamy haifai kabisa kwani itawatesa wanaume wengi watakosa wake. Na itachochea umalaya badala ya kuupunguza. Wanaume watakaokosa wake watawategemea malaya. It will be a vicious circle.
Niwadokeze kidogo. China walipokuwa na sera ya mtoto mmoja mmoja. Kwa kuwa wanaume ndio wanapendwa wazazi wengine waliwaua watoto wa kike kusudi wapate wa kiume wanaopendelewa. Kwa hiyo China kuna uhaba mkubwa wa wanawake hadi wanatekwa nyara hata wale walioolewa na kupelekwa vijijini.
Kwa hiyo hamsini kwa hamsini na mme mmoja mke mmoja ndio ushauri wangu.
Nawasilisha kwa mjadala zaidi na kukosolewa kama nimekosea. With data plz.
Mama T
Forwarded as received.