Kwa familia ambazo zimeingia na kuamini dini za Kikristo na Kiislamu, mila hizo hazina nguvu na hazifuatwi. Lakini kwa wanaoamini mila na desturi hizi, Lichumu na Emisilo zina nguvu sana na wanapata madhara wasipofuata.”
Lichumu na Emisilo haiwatengi mume na mke pekee wanapofiwa, bali hata watoto ambao wazazi wao wamefiwa.
Alipoulizwa kuhusu mila hizo, mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella hakutaka kuzungumzia masuala hayo ya kiimani na kimila zaidi ya kuwataka wananchi wajiepushe nayo.