Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"


Asee kwenye utawala wa Mwalimu kulikua ufisadi wa kiwango cha juu. kulikuwa kigogo mmoja anaitwa Boniventura Chambaka, huyu jamaa alikuwa anaaminiwa kuongoza kampuni kubwa kubwa, lakini alizifisadi sana. Mara utasikia ametolewa UFI kapelekwa Aluminium Afrika, ALAF, ukitokea msala utasikia kahamishiwa Urafiki, akikinukisha utasikia yupo Kiwanda cha mbolea Tanga, Akivuruga utasikia yupo Twiga Cement. Na mwenzake alitwa Yesaya Mwailolo wa Bora. Ni ufisadi juu ya ufisadi. Na kwakuwa wakati ule hakukuwa na vyombo vya habari kama ilivyo leo hakukuwa na wa kumkosoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…