Bobby Greenlease
Ivan aliokolewa akiwa hai, lakini Bobby Greenlease kijana mwenye umri wa miaka 6, mtoto wa milionea mfanyabiashara wa magari Robert Cosgrove Greenlease aliacha msiba kwa familia.
Septemba 28, 1953, watumiaji dawa za kulevya Carl Austin Hall na Bonnie Emily Brown Heady walipanga kumteka mtoto asiye na hatia. Heady alijifanya kuwa shangazi wa mvulana huyo, na akamshawishi mtawa katika shule ya Bobby amruhusu mapema, akisema familia ina jambo la dharura.
Kati yao Hall alisoma darasa moja na baba yake Bobby, na alikuwa amepanga miaka mingi kuidhuru familia ya Greenlease. Hivyo, wawili hao walimchukua Bobby wakaenda naye hadi Kansas ambako walimpiga risasi kwa bastola akafa.
Baada ya mauaji, walitaka walipwe kikombozi cha dola 600,000. Familia ya Greenlease ikihaha kumuokoa mtoto wao hawakujua tayari alikuwa amekufa, wakalipa. Haikuchukua muda mrefu kwa mamlaka kubaini ukweli na wawili hao walikamatwa, wakashtakiwa na wakanyongwa mwaka 1953.