Kashfa ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni zikiwemo za kusisimua misuli imezidi kuathiri mchezo huo nchini Kenya.
Hiyo inatokana na kufungiwa miaka minne kujihusisha nariadha kwa mwanariadha chipukizi wa mbio ndefu za marathon, Samuel Kalalei baada ya kufeli vipimo vya damu.
Mwanariadha huyo mwenye miaka 23, alifeli vipimo alivyofanyiwa Aprili mwaka huu katika mbio za Rotterdam Marathon nchini Uholanzi.
Kalalei, alikuwa akijiandaa kujiwekea muda bora zaidi katika mbio ndefu baada ya mwaka jana kutwaa ubingwa wa Athens Marathon.