Mara ya mwisho nilipewa maelezo haya na Guide mmoja nikiwa serengeti,
Kwamba mto huu Masai mara kwa asili unafanya uwiano wa idadi ya wanyama wala nyasi hasa punda milia nyumbu/nyati n.k.
Alisema wanyama wanapo hama kukatizaq mto Masai mara, ni asilimia 50% tu hufaulu kuvuka! Wengine wote huwa chakula ya mamba na kiboko mtoni.
Kipindi hicho ni kipindi ambacho wanyama hao kwa kiasi kikubwa ni wajawazito/wana mimba, kwa hivyo ile 50% ilovuka mto huzaliana tena ku-cover idadi ya wanyama walioshindwa kuvuka Masai mara.
Huu mto unastory nzuri kuskia na matokeo chanya kwa viumbe wote, yaani wa nchi kavu na wale waishio majini kama mamba na kiboko.