Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kabla ya kuwa rais wa Ethiopia, Bi Sahle-Work alikuwa mwakilishi wa UN katika Umoja wa Afrika
Kwa mujibu wa katiba ya Ethiopia , rais hana nguvu ikilinganishwa na wadhifa wa waziri mkuu ambaye yeye ndiye, aliye na nguvu za kisiasa nchini.
 
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011.
Alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia.
 
Saara Kuugongelwa-Amadhila aliteuliwa waziri mkuu wa Namibia mnamo 2015, akiwa amewahi kuwa waziri wa fedha kwa miaka kadhaa.
Akiwa na mwanachama wa muda mrefu wa chama cha South West Africa People's Organization (SWAPO), alikuwa uhamishoni Sierra Leona akiwa katika chama hicho akiwana umri wamiaka 13.
Baada ya kuhitimu katika chuo kikuu Marekani Bi Kuugongelwa alirudi Namibia na kufanya kazi kwa muda mfupi katika ofisi ya rais wa kwanza Sam Nujoma.
 
Ameenah Gurib-Fakim, aliwahi kuwa rais wa Mauritius kabla ya kujiuzulu kufuatia mzozo wa kifedha uliokuwa unamkabili.
Alituhumiwa kutumia kadi ya fedha aliyopewa na shirika la misaada kununua vitu vya kibinfasi vyenye thamani ya maelfu ya dola.
Bi Gurib-Fakim ni mwanasayansi tajika na mnamo 2015 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika wadhifa wa rais wa Mauritius.
 
Daraja la Mufunje ni eneo maarufu mno kwa wenyeji wa eneo la Nzoia magharibi mwa Kenya.
Daraja hilo ambalo limejengwa kwa nyaya pamoja na mbao na linaviunganisha vijiji viwili, wale wanaoishi upande wa Nzoia na wale walioko upande wa Bukoba.
Jina Mufunje lina maana ya kufunganisha kitu pamoja, maana inayo endana sawa na muonekano wa daraja lenyewe.
 
Lakini kwa macho ya mgeni, moja kwa moja hisia ya hatari hukujia unapolitazama daraja hilo.
Ni kivukio kikuu kwa wakaazi wa eneo hilo, wazee kwa vijana wanaoonekana wakivuka pasi kuhisi hatari ya mto unaopita chini ya daraja hilo ulio na wanyama hatari kama mamba.
Mwandishi wa BBC Anne Ngugi aliyefika katika eneo hilo anasema, kila mtu analenga safari yake kuvuka hadi ng'ambo nyengine.
Na ni hapa ambapo pia alishuhudia mama mmoja kwa jina Metrin Midinyo akiwa na mtoto wake mngongoni akivuka.
 
Metrin anasema kuwa yeye haogopi wala hana wasiwasi wowote wa kuvuka daraja hili , japo anakubali kuwa mara kwa mara nyaya za daraja hili huoza na kukatika.
Anaeleza kwamba pia mbao zenyewe huoza na hutokea mtu huenda akajipata ameanguka katika mto Nzoia unaopita chini, mojawapo ya mito mikubwa nchini Kenya.
 
?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1s43jf53o7jya.jpg
 
Patrick Wekesa ana miaka 25 anaeleza kuwa tangu utotoni mwake akikumbuka mwaka wa 1995 yeye pamoja na watu wa jamii yake walikuwa wanatumia daraja hilo.
Yeye ni fundi wa mbao , kila siku yeye huvusha mbao kupitia daraja hilo la Mufunje kutoka upande mmoja hadi mwengine.
Sio hayo tu, anasema kuwa yeye hawezi kumudu kupita njia mbadala ambayo humgharimu takriban dola karibu 5 kupita njia nyingine ambayo ni ndefu mno.
Daraja hili la Mufunje linaunganisha vijiji ambavyo vinahitajiana mno.
 
Back
Top Bottom