Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20181027-WA0014.jpg
 
Mshambuliaji mahiri wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, amechochea moto kwenye pambano la mahasimu wa Hispania ‘El Clasico’ akisema Barcelona itaichapa Real Madrid kesho Jumapili licha ya kukosekana kwa nahodha wake Lionel Messi.

Alisema Real iliyomkosa Cristiano Ronaldo aliyeondoka na kujiunga na Juventus, imepoteza ubora hususani katika safu yake ya ushambuliaji, hivyo hana shaka kuwa itapoteza mchezo huo.
 
Alisema mchezo huo utakaochezwa kwa mara ya kwanza bila kuwa na nyota hao ambao kwa miaka tisa mfululizo walikuwa wakiamua matokeo ya mechi za El Clasico, italazimika kuamuliwa na timu itakayocheza kitimu zaidi na ndiyo sababu anaipa nafasi Barcelona.

Messi mwenye 30, ambaye atakosekana kwenye mchezo huo baada ya kuvunjika mkono, anaongoza katika historia ya muda wote ya mabao katika mechi za El Clasico akiwa amefunga mabao 26 katika mashindano tofauti.
 
Ronaldo ndiye anayeshika nafasi ya pili akiwa na mabao 18, wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na nahodha wa zamani wa Real, Raul mwenye mabao 15, wakifuatiwa na magwiji wa zamani wa Real Francisco Gento na Ferenc Puskas ambao kila mmoja amefunga mabao 14 sawa na yota wa zaamni wa Barcelona, Cesar.

Timu hizo zitakuwa zinakutana katika mchezo wa 178 wa La Liga katika mechi 177 walizokutana Real imeshinda 72, Barcelona 70 zimetoka sare 35 na kwa ujumla zimekutana katika michezo 239 za mashindano mbali mbali.
 
Back
Top Bottom