Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya bao la mshambuliaji Danny Welbeck, kuipa Arsenal ushindi wa 11 mfululizo walipoilaza Sporting Lisbon ya Ureno kwa bao 1-0 na kukaa kileleni mwa kundui E la Europa Ligi, kocha Unai Emery, amefunguka.

Emery alimpa sifa Welbeck aliyetumia vema makosa ya Sebastian Coates na kuukwamisha mpira wavuni katika dakika ya 77 ya mchezo, akifanya Arsenal kushinda mechi 11 mfululizo za michuano mbali mbali msimu huu.
 
Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Arsenal kushinda ugenini nchini Ureno imeshacheza mara tatu na kupoteza zote, hata sio Arsenal tu bali hakuna timu iliyoondoka na pointi tatu msimu huu kwa timu za Uturuki.

Kwa ujumla kocha Emery, ameonekana kuanza kupata mafanikio na timu haishii kupata matokeo mazuri bali hata katika uchezaji timu inacheza soka la kuvutia.
 
Katika mchezo huo kocha Emery alifanya mabadiliko ya wachezaji sita kati ya wale wa kikosi cha kwanza akilenga kuwapumzisha kwa ajili ya kuweka nguvu katika mchezo ujao wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace utakaopigwa ugenini kesho.

Aidha huo ulikuwa ni muendelezo wa ushindi kwani ilitoka kuishinda Leicester City kwa mabao 3-1 katika Ligi Kuu England na kuchupa hadi nafasi ya nne katika msimamo ikifikisha pointi 21 sawa na Chelsea na Tottenham, zikiwa pointi tatu nyuma ya vinara Man City na Liverpool.
 
Katika mchezo huo wa kundi E, winga wa zamani wa Manchester United Nani aliipotezea Sporting nafasi muhimu ya kupata bao la kuongoza lakini akashindwa kuituma nafasi hiyo.

Arsenal ilijibu shambulizi hilo katika dakika ya 32 pale mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Henrikh Mkhitaryan, kumbabatiza kipa Renan Ribeiro kutolewa.
 
Wakati huohuo Bosi wa United Jose Mourinho anataka wachezaji wake wajumuike naye kutembea kutoka Hotelini mpaka Uwanjani Old Traford kukwepa foleni inayoweza kutokea kama ilivyotokea kwenye mchezo dhidi ya Juventus kwenye UEFA ingawa watu wa usalama nchini humo wamepinga zoezi hilo. (Mail)
 
Bosi wa Newcastle Rafael Benitez, anaweza kuwa nje ya mkataba katika kipindi cha kiangazi, hivyo amependekeza kuwa anaweza kuiongoza timu katika msimu ujao licha ya kuwa timu hiyo iko katika kiwango cha chini katika ligi za Premia. (Mirror)
 
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, alisikitishwa kwa kutoitwa katika kikosi cha England kilichoenda kwenye kombe la dunia hivyo amekata tamaa kuichezea tena nchi yake. (Telegraph, subscription required)
 
Klabu ya Manchester United bado imeendelea kuwa na mipango ya kumsaninisha beki wa pembeni raia wa Hispania Jordi Alba, 29, kwenye dirisha la usajili la mwezi January ambapo itachukua mpaka mwisho wa msimu kwa Fc Barcelona kumuongeza mkataba mpya beki huyo (Diario Sport - in Spanish)
 
Back
Top Bottom