Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
 
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
 
Unatakiwa kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa miguu kwa umbali mrefu.
 
KUNA watu wanataka kuvisha macho yao lakini hawana uwezo, wapo wanaotaka midomo yao kuwa minene zaidi na hana uwezo .Kwani kuna watu wanaangalia televisheni na kusema ngoja niwe kama yule au anasoma katika picha na kusema nataka kuwa hivi. Wacha mambo hayo usijilinganishe na mtu yoyote yule, jitambue na hakikisha kwa kujitambua kwako unajitengenezea kuwa mrembo zaidi
Kioo huchangia kuimarisha
 
Kitu kimoja kizuri kinachorekebisha sana desturi na kitu unachotaka ni kioo. Wanawake wengi wanakwepa kujiangalia katika kioo wanaona kioo kinawapa kitu cha siri wasichotaka kujua. Kioo kinaweza kuwa rafiki yako mkubwa na kioo kinaweza kukuambia unaendeleaje kioo kinakupa kitu ambacho macho hivi hivi hayawezi kuona.
 
Fanya kila kitu vizuri
Namna unavyotumia vikolozo vyako vya uzuri kwa namna inayostahili ndivyo utakavyopata matokeo unayoyataka.
Mathalani fanya kama wanavyofanya watu wa saluni unapoenda kutengeneza nywele utaona kwamba shampoo haimwagwi kichwani bali inatiwa katika mikono na kupelekwa kichwani mwako kama kusikasuka.
Fanya masaji ya nywele wakati unatengeneza nywele halafu osha vyema na nyanyua nywele zako mpaka zinakubaliana na wewe.
 
44328398_487492641748038_7345857851201223412_n.jpg
 
Mradi wa ulimbwende
Jisikie bomba, jisikie maridadi , ukijisikia mbaya ujue ndivyo dunia itakavyokuona na ukijisikia bomba ndiyo dunia itakuona bomba.
Marafiki wanaofaa
Wanachosema watu kama kwa makusudi au la ni dhahiri hukusaidia kujisikia vyema au vibaya, tafuta marafiki wanaokufanya ujisikie vizuri si wale wanaokufanya utake kujua.
 
Jisikilize
Jisikilize mwenyewe kwani hicho ndiyo hasa kitakachokufanya ujisikie vyea na kuendelea na mambo yako vyema. Kujisikia kunasuuza sana akili, tafuta muda wa kujisikiliza mwenyewe hiki ni kipindi cha kuona mambo yalivyo.
 
Back
Top Bottom