Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
4286.jpeg
 
Wachezaji wa Chelsea, Ross Barkley na Antonio Rudiger, walishindwa kuungana na wenzao kurudi London kutoka Burnley kutokana na kushindwa kutoa kipimo cha mkojo baada ya mechi yao dhidi Burnley.
Wachezaji walikuwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichoichapa mabao 4-0 Burnley, kwenye Uwanja wa Turf Moor na kuendeleza mwanzo wa kishindo wa Chelsea katika Ligi ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi kumi.
 
Barkley mfungaji wa bao la pili la Chelsea na mpishi wa bao jingine pamoja na Rudiger ndio wachezaji pekee kwa upande wa Chelsea waliochaguliwa kupimwa ili kujua kama wanatumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Katika hali ya kushangaza wachezaji hao wote walishindwa kupata mkojo uliohitajika mbele ya maofisa wa wakala wa kupiga vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni, hivyo ikabidi wapewe vimimikika kwa wingi na kusubiriwa kwa muda.
 
Maofisa wa wakalawa vipimo hivyo, waliueleza uongozi wa Chelsea tatizo lililojitokeza na kwamba wasingewaruhusu kuondoka kabla ya kukamilisha zoezi hilo la kutolewa mkojo kwa kila mmoja wao.
Baada ya msimamo huo, msafara wa Cheslea uliwasubiri kwa nusu saa na kuamua kuondoka ukiwaacha wachezaji hao ambao walitumia saa mbili zaidi kufanikisha utoaji wa mkojo kwa ajili ya vipimo.
 
Back
Top Bottom