Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Defour jana Jumapili alitarajia kuwapo uwanjani kuwakabili Chelsea kwenye Ligi Kuu England na kusema kwamba anachofahamu kwa muda ndoto za Hazard ni kwenda kujiunga na Real Madrid. Kwa muda sasa, Hazard amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Real Madrid huku mwenyewe akiwahi kukiri kwamba ndoto zake siku moja kwenda kuwatumikia wababe hao wa Bernabeu. Hazard bado hajaamua kusaini mkataba mpya kwenye kikosi cha Chelsea na jambo hilo linachochea taarifa za kwamba huenda akaondoka kwenye timu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge