Wachezaji wa Chelsea, Ross Barkley na Antonio Rudiger, walishindwa kuungana na wenzao kurudi London kutoka Burnley kutokana na kushindwa kutoa kipimo cha mkojo baada ya mechi yao dhidi Burnley.
Wachezaji walikuwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichoichapa mabao 4-0 Burnley, kwenye Uwanja wa Turf Moor na kuendeleza mwanzo wa kishindo wa Chelsea katika Ligi ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi kumi.