Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KUONYESHA ukubwa wao, katika ziara ya Rais wao, popote duniani, Wamarekani zaidi ya ulinzi mkubwa lakini wanataka kuonyesha ukubwa wao. Itashuka Air Force One, watashuka Mbwa, zitashuka Manowari. Rais wenu atafanya kuwa raia wa kawaida tu.

Waingereza kitu hiki wanakiita Fear factor. Wanatengeneza hofu. Hofu dhidi ya adui au mtu mwingine ambaye yupo tofauti nao. Wakati mwingine hata kwa yule ambaye yupo upande wao. Mnabakia na hofu muda wote kuhusu ukubwa wao.
 
Real Madrid walimtumia Cristiano Ronaldo hivi. Zaidi ya matangazo ya biashara na mikataba anayoingiza klabuni, zaidi ya mabao yake yanayowapa ubingwa. Kuna kitu kilijengeka kuhusu Ronaldo. Anatia hofu. Anatisha.

Wachezaji wa timu pinzani na benchi lao la ufundi, na mashabiki wao, na matajiri wao, wanapofikiria kwamba wanakwenda kucheza na Real Madrid kwa asilimia kubwa wanafikiria kwamba wanakwenda kucheza na Ronaldo. Hofu inawajaa. Wanapoteza uwezo wa kujiamini.
 
Barcelona wanamtumia Lionel Messi hivi. Hata Chelsea wanamtumia Eden Hazard hivi. Adui anaogopa kivuli cha Ronaldo kupitiliza. Hata kama Ronaldo hayupo katika fomu lakini kivuli chake kinatisha wapinzani. Hii ndio maana halisi ya Fear factor.
 
Kuondoka kwa Cristiano kwenda Juventus ni tatizo kwa Madrid. Wapinzani kwa sasa hawataiogopa Madrid. Zamani walikuwa wanaogopa hata kivuli chake. Mpango wa kwanza wa kocha wowote ule ni namna ya kumdhibiti Ronaldo. Mpango wa pili ni namna ya kuidhibiti Madrid. Mpango wa tatu ni namna ya kushinda mechi yenyewe.
 
Hii ndio faida ambayo wakati mwingine Madrid walikuwa wanaipata kwa kuwa na Ronaldo uwanjani. Mtu aliyepata mataji matano ya mwanasoka bora wa dunia hakuyapata bure. Alikuwa hatari uwanjani. Alitengeneza hofu kuu kwa wapinzani.
 
Kuondoka kwa Ronaldo sasa hivi kunawafanya akina Real Sociedad, Granada, Valencia na wengineo waione Madrid kama timu nyingine ya kawaida. Hili ndio tatizo la kuwa na mchezaji ambaye amewaacha mbali zaidi wenzake kwa uwezo.
 
Hili ndio tatizo la kutengeneza timu ambayo zaidi ya uhatari wa mtu mmoja, lakini kinyume chake hakuna timu yenye maelewano makubwa ambayo imeundwa. Barcelona walijitahidi wakati wa Pep Guardiola. Hata kama Messi na ukubwa wake asingekuwepo uwanjani lakini akina Xavi Hernandez, Sergio Busquets na Andres Iniesta walikuwa watu hatari na wangeweza kutengeneza nafasi nyingi.
 
Nje ya Ronaldo Madrid imeonekana kuwa timu ya kawaida. Sababu ni hizi tatu. Kwanza hawana timu yenye kombinesheni ya uhakika, pili unakosa ubora wa Ronaldo, tatu wanakosa tu uwepo wa Ronaldo uwanjani hata kama hayupo fomu.
 
Hili la tatu ndilo ambalo linazipa timu nyingi kujiamini. Wakati timu zinatoka katika vyumba vya kubadilishia nguo na Ronaldo haonekani, kocha wa timu pinzani anatazama wachezaji wa Madrid na kuona kama vile anaitazama Valencia au Sevilla. Huu ndio ukweli mchungu ambao utawasumbua Madrid kwa muda mrefu.
 
Haliwezi kuwa tatizo la kudumu lakini kwa sasa linawatusmbua kidogo Madrid mpaka watengeneze timu nyingine ambayo itaziba pengo la Ronaldo. Bahati nzuri yenyewe ni kwamba pengo la Ronaldo halitazibwa kwa kumtafuta Ronaldo mwingine. Litazibwa kwa timu kuundwa kwa mfumo wa kitimu zaidi.
 
Hakuna mchezaji ambaye nyakati zake hazipiti. Kabla ya Ronaldo kulikuwa na mastaa wengi tofauti Madrid na walicheza kwa staili tofauti na ile ya Ronaldo lakini bado Madrid ilitamba. Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu. hata hivyo inahitaji muda kidogo kwa timu kujipanga upya.
 
Mbaya zaidi kwa Madrid ni kwamba nje ya Ronaldo bado wachezaji wao wengi mahiri sio damu changa. Barcelona Jumamosi walishinda mabao 5-1 wikiendi iliyopita dhidi ya Madrid na ungeweza kuona damu yao changa ni bora kuliko ile ya Madrid.
 
Kwao ni rahisi kucheza bila ya Messi kuliko ambavyo Madrid wanaweza kucheza bila ya Ronaldo. Na kama wasingemuuza Neymar kwenda PSG ndio ingekuwa rahisi zaidi kwao kucheza bila ya Messi kuliko Madrid kucheza bila ya Ronaldo.
 
Kabla hata Ronaldo hajaondoka, au mara tu baada ya Ronaldo kuondoka, Florentino Perez alipaswa kuwachukua watu kama akina Eden Hazard, Mauro Icardi, N’Golo Kante na wengineo kwa ajili ya kuitia timu chaji. Hakufanya hivyo.
 
Mchezaji wa mwisho tishio kumchukua alikuwa Gareth Bale katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2013. Kuanzia hapo alikuwa anachukua wachezaji wa wastani. Sijui Perez amekumbwa na ugonjwa gani wa ubahili ambao ulikuwa haujawahi kumtokea maishani.
 
Back
Top Bottom