Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
.MBIO za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England inazidi kuwa kali kila wiki. Liverpool na Chelsea zinapambana kwelikweli kwa sasa kujaribu kuwabana Manchester City kwenye mbio hizo za ubingwa.

Arsenal na Tottenham Hotspur mambo bado, lakini kwamba hawamo kwenye mbio hizo. Jose Mourinho na chama lake la Manchester United ni wazi kabisa suala la kuwa bingwa itakuwa nguvu kwake, lakini kitu anachoweza kukifanya ni kupambana kuwamo kwenye Top Four.
 
Katika kuhakikisha mbio hizo zinakuwa zenye ushindani mkubwa ndio maana kila timu inajaribu kutafuta namna ya kufunga mabao kwa maana ya kupiga mashuti mengi. Hizi hapa ni timu sita zinazoongoza kwa kupiga mashuti kwenye Ligi Kuu England baada ya mechi 10 kuchezwa.
 
6.Man United- mashuti 133

Kocha Jose Mourinho anahitaji kutafuta tiba ya kuondoa ugonjwa unaokabili timu yake kwanini inashindwa kufunga mabao ya kutosha.

Timu hiyo imepiga mashuti mengi sana, imepiga 133, lakini cha ajabu imefunga mabao 17 na kujikuta wakishika nafasi ya nane huko kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Man United wamefunga mabao 17, wamefungwa 17 wana pointi 17. Kwa msimu huu wamepiga mashuti mengi na kuongia kwenye orodha ya timu zilizopiga mara nyingi mashuti katika mechi 10 ilizocheza kwenye ligi, lakini mabao waliyofunga ni aibu.
 
5.Everton-mashuti 137

Everton walikaribia kabisa kupata pointi huko Old Trafford wikiendi iliyopita wakati ilipokwennda kumenyana na Manchester United.

Wababe hao wa Goodison Park walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 mapema tu, lakini kwenye kipindi cha pili walicharuka na kupata bao moja, huku ilibaki kidogo tu wasawazishe. Kocha Marco Silva bila ya shaka atakuwa mtu mwenye huzuni kwa kuona timu yake imefunga mabao 16 tu kutoka kwenye mashuti 137 iliyopiga. Everton kwa sasa wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi hiyo na pointi zao 15.
 
4.Liverpool-mashuti 145

Liverpool wamelingana pointi na Manchester City kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, wote wakiwa kileleni kwenye msimamo, lakini chama la Pep Guardiola linaongoza kwa kuwa na mabao mengi.

Kwenye Ligi Kuu kwa mechi 10 ilizocheza hadi sasa, Liverpool imepiga mashuti 145 na 20 tu ndiyo yaliyotinga kwenye nyavu kuwa mabao.
 
Kitu kizuri kwao ni kwamba wameruhusu mabao manne tu kwenye nyavu zao. Katika kuepuka lile lililotokea mwaka 2012 kuhusiana na mabao, kikosi hicho cha Jurgen Klopp kimeanza msimu huu kwa kasi moja tu ya kufunga mabao. Wolves nao wamepiga mashuti 145 na kufunga mabao tisa tu.
 
3.Southampton- mashuti 146

Kocha Mark Hughes yupo kwenye presha kubwa huko Southampton. Tatizo kubwa la kocha huyo wa zamani wa Stoke City na Manchester City ni kufunga mabao. Southampton inashika namba tatu kwa kupiga mashuti mengi kwenye Ligi Kuu England, lakini wamefunga machache sana.

Wamepiga mashuti 146 na wamefunga sita tu. Wanashika nafasi ya 16 kwenye msimamo na pointi zao saba.

Kazi ya Hughes inayomkabili kwa sasa ni kutengeneza safu yake ya ushambuliaji kuwa kali ili kuokoa jahazi. Ni jambo linaloshangaza kidogo na gumu kuelewa kukosa mabao kwenye timu yenye washambuliaji kama Charlie Austin, Manolo Gabbiadini, Shane Long na Danny Ings.
 
2.Chelsea-mashutu 187

Chelsea waliwachapa Burnley 4-0 wikiendi iliyopita kurudi kwenye mwendo wao wa kushinda baada ya kupata sare ya kibahati mbeye ya Manchester United wiki mbili zilizopita.

Kikosi hicho cha kocha Maurizio Sarri kinaonekana kuwa vizuri kwa sasa baada ya kuonekana wachezaji wake wa kutoka kila idara wakifanya vizuri.

Chelsea ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kama mashuti yake yote iliyopiga 187 kwenye mechi 10 walizocheza kwenye ligi yangetinga nyavuni. Chelsea imefanikiwa kufunga mabao 24 na kufungwa saba. Wanashika namba tatu kwenye msimamo na pointi zao 24.
 
1.Man City-mashuti 211

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City msimu huu si kwamba wapo wakali sana kwa kulinganisha na ule uliopita, lakini kiwango chao kipo vizuri na wapinzani wake wanaomfukuzia, Liverpool na Chelsea wanaonekana pumzi zimeshaanza kukata.

Kocha Pep Guardiola ameweza kukifanya kikosi chake kushinda mechi hata kama hakichezi vizuri.
 
Kwa sasa wamekusanya pointi 26 kama ilivyo kwa Liverpool, lakini wao wapo kileleni kwa tofauti ya mabao. Wamefunga mabao 27.

Lakini, kikubwa ni kwamba Man City wameonyesha uchu wa kufunga mara nyingi zaidi msimu huu na ndio maana wamepiga mashuti 211 hadi sasa kwenye ligi hiyo.
 
.MMOJA kati ya mastaa wa Barcelona walioimaliza kabisa Real Madrid katika pambano la wikiendi iliyopita ni staa mpya wa Barcelona, Arthur Melo ambaye jina lake linazidi kuvuma kwa kasi Nou Camp tangu atue klabuni hapo katika dirisha kubwa la majira ya joto akitokea Gremio. Ni nani huyu Arthur?
 
Aibuliwa na Luiz Felipe Scolari.

Jina lake halisi ni Arthur Henrique Ramos de Oliveira Melo na alizaliwa Agosti 12, 1996 katika eneo la Goiania nchini kwao Brazil. Arthur alianza kucheza soka katika klabu ya mtaani kwao ya Goias akiwa na umri wa miaka 12.

Hata hivyo, mwaka 2010 maskauti wa klabu ya Gremio inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil walimuona katika michuano ya vijana na kufanikiwa kumnasa. Januari 2015 baada ya kutesa katika michuano ya vijana ya jimbo la Sao Paulo, Arthur alipelekwa katika kikosi cha kwanza na kocha wa Gremio, Luiz Felipe Scolari.
 
Bila ya kutazamia alicheza mechi yake ya kwanza katika michuano ya Jimbo dhidi ya Aimoré. Hata hivyo alitolewa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na mlinzi wa Argentina, Matias Rodriguez. Hakucheza tena mechi za wakubwa msimu huo.

Mwaka 2016, Arthur alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi katika pambano Botafogo walilochapwa 1-0 akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kaio katika kipindi cha pili. Mwaka 2017 alikuwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha kwanza.
 
Uki-like comment hii unapata like 5
IMG_20181029_224813.jpg
 
Katika pambano lake la kwanza la klabu bingwa Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores lililoisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Guarani, Arthur alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya kufikisha pasi zote 40 alizopiga.

Alifunga bao lake la kwanza katika soka la kulipwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fluminense kombe la Brazil. Julai alifunga bao lake la kwanza la Ligi katika ushindi wa mabao 3-1 wa Gremio ugenini dhidi ya Vitoria.
 
Back
Top Bottom