Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Afananishwa na Iniesta, Barca yamnasa

Aina yake ya soka imekuwa ikilinganishwa zaidi na viungo mahiri wawili wa Hispania, Andrés Iniesta na Thiago Alcântara. Arthur ana kipaji kikubwa katika umiliki wa mpira pamoja na kupiga pasi fupi na ndefu ambazo zimempatia umaarufu mkubwa.

Klabu kubwa za Ulaya, Chelsea, Manchester United na Barcelona zote zilikuwa zinamfukuzia kwa karibu Arthur lakini ni Barcelona ndio ambao walifanikiwa kuinasa saini yake kwa dau la Euro 40 milioni.
 
Kabla ya hapo Kocha wa United, Jose Mourinho aliwatuma maskauti wake kwenda kutazama kipaji cha Arthur huku Chelsea nayo ikimtazama kwa karibu lakini kwa mujibu wa Mwandishi nguli wa soka la Hispania, Guillem Balague atoa siri kwamba Barcelona wamefikia makubaliano ya kumnasa kinda huyo.

“Arthur ana makubaliano na Barcelona, lakini inahitaji kuthibitishwa na Gremio ambayo inataka ilipwe kiasi cha Pauni 44 milioni kwa ajili ya kumruhusu aondoke. Kiasi hicho kipo katika kipengele cha mkataba wake.” alisema Balague.
 
Taarifa nyingine zilidai kwamba siku mbili baada ya kuisaidia Gremio kutwaa taji lake la tatu la Copa Libertadores, Arthur pamoja na wakala wake, Andre Curry walikutana na Maofisa wa Barceona katika mji wa Porto Alegre kujadili zaidi uhamisho wa staa huyo.

Hata hivyo utata ulizuka baada ya picha kuibuka zikimuonyesha Arthur akiwa na jezi ya Barcelona kando ya Baba yake, wakala wake na mfanyakazi mmoja wa wakala wake. kitu hicho kiliichukiza Gremio ambayo ilisisitiza kwamba staa huyo angeondoka kwa dau lililopo katika mkataba wake tu ingawa Barcelona walitaka kulipa dau la chini.
 
baadaye Gremio ilisisitiza kwamba isingemruhsu nyota huyo kuondoka Brazil kabla ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Russia mapema mwaka huu

Machi 11, 2018, Barcelona ilifikia makubaliano na Gremio kuhusu uhamisho wake kwenda Nou Camp na alisaini mkataba wa miaka sita huku akilazimika kusubiri mpaka Julai 9, 2018 kuwa mchezaji rasmi wa Barca. Alicheza mechi yake ya kwanza kwa Barca katika pambano la maandalizi ya msimu dhidi ya Tottenham mnamo Julai 28 na kufunga bao lake la kwanza katika pambano hilo.
 
Yumo kikosi cha Brazil

Arthur ameichezea Brazil katika ngazi zote. Ameichezea katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17 na kile cha chini ya umri wa miaka 20. Alikuwa seheu ya kikosi cha Brazil chini ya umri wa miaka 17 kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Amerika Kusini chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2013.

Septemba 15 mwaka huu, Arthur baada ya kung’ara zaidi na kikosi cha Gremio aliitwa katika kikosi cha wakubwa cha Brazil ambacho kilitarajiwa kucheza mechi mbili za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Bolivia na Chile.
 
Arthur alikuwepo katika kundi la wachezaji wa akiba kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia nchini Russia mapema mwaka huu. hakuweza kwenda Russia kutokana na timu hiyo kupata majeruhi katika eneo la kiungo.
 
Kila baada ya dakika moja umecomment

Macommenti marefuuu

Unaandikaa? Au unacopy?
IMG_20181029_224852.jpg
 
SOKA limebadilika sana katika miaka 10 ya hivi karibuni hasa baada ya kuibuka kwa mitandao ya kijamii. Klabu zote kubwa na mastaa wa maana wamekuwa wakitengeneza pesa nyingi sana ndani na nje ya uwanja.

Kitu wanachokifanya wachezaji kwa sasa ni kuhakikisha wanapatikana kwenye mitandao hiyo ya kijamii wakifanya majina yao kuwa nembo kubwa ili kupiga pesa. Masupastaa makini kama Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic wametumia faida ya umaarufu wao kujitengeneza kama nembo zinazopiga pesa nyingi na kuwa matajiri wakubwa. Hawa hapa mastaa waliotumia umaarufu wa majina yao kuwa nembo za kibiashara.
 
7.Mesut Ozil– MO Brand

Staa wa Arsenal, Mesut Ozil amewazidi ujanja wachezaji wenzake wengi tu huko Emirates. Linapokuja suala la kupiga pesa nyingi nje ya mshahara, Ozil amewaacha mbali wenzake huko kwenye kikosi cha Arsenal. Mjerumani huyo ametumia jina lake kama nembo na kuzindua logo yake inayokwenda kwa jina la MO. Akiwa na kampuni hiyo, Ozil, aliyewahi kuichezea pia Real Madrid amekuwa akifanya biashara ya kuuza kofia na fulani kwa kupitia kampuni yake ya mitindo. Staa huyo amekuwa akipiga pesa pia kutoka kwa Adidas, Toyota, na Pro-Evolution Soccer (PES) kwa kupitia nembo yake hiyo
 
6.Paul Pogba– PP Brand

Supastaa wa Manchester United, Paul Pogba amekuwa akikosolewa kila siku kwamba haweki juhudi kubwa anapokuwa ndani ya uwanja ili kuisaidia timu yake. Wachezaji wakongwe kama Paul Scholes wamekuwa wakimshambulia sana kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Lakini, mchezaji huyo ghali wa Man United haonekani kujali hizo kelele za watu. Anaacha tu mambo yake yazidi kuwa mazuri ndani na nje ya uwanja, ambapo staa huyo ameanzisha nembo yake ya kibiashara inayoitwa kwa jina la PP. Unaweza kujiuliza kwanini Pogba amekuwa akibadilisha mitindo yake ya nywele kila wakati, lakini hafanyi hivyo kwa kujifurahisha hiyo ni biashara. Nembo yake ya PP kwa kushirikiana na Adidas wamekuwa wakitengeneza kofia pamoja na viatu.
 
5.Lionel Messi– Messi Brand

Lionel Messi amekuwa si mtu mwenye kutafuta umaarufu sana kama ilivyo kwa wapinzani wake Cristiano Ronaldo na Neymar. Staa huyo wa Kiargentina amekuwa na umaarufu mkubwa sana ndani ya uwanja na huko amefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Lakini, kung’ara uwanjani kumemfanya Messi jina lake kuwa nembo kubwa kibiashara. Mwaka 2011 alizindua logo ya nembo yake hiyo na kusema hiyo ndiyo itakayokuwa ikimtambulisha kwenye mambo yake yote. Nembo hiyo imezidi kumfanya Messi kupiga pesa nyingi nje ya uwanja hasa kutokana na kunasa dili za kibiashara na kampuni za Gatorade, Huawei Technologies, Adidas na Tata Motors.
 
4.Zlatan Ibrahimovic– Zlatan Brand

Zlatan Ibrahimovic wala hahitaji kutambulishwa kutokana na jinsi alivyochezea timu nyingi na kubwa huko Ulaya. Fowadi huyo mwili jumba kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha LA Galaxy ya huko Marekani. Lakini, kabla ya hapo alipita Barcelona, AC Milan, PSG, Inter Milan, Juventus, Ajax na Manchester United. Ibra alitumia umaarufu wake kuanzisha miashara yake ya mavazi inayofahamika kwa jina la A-Z Sportswear. Staa huyo wa Sweden pia ana pafyumu yake ambayo inachuana na ile ya CR7. Tangu alipotua Marekani, kampuni kubwa kama ya Samsung imetumia nembo yake kujitanua zaidi kibiashara.
 
3.Neymar Jnr.- INJR Brand

Neymar anaonekana kujifunza kwa kasi sana kutoka kwa Cristiano Ronaldo. Wawili hao walikuwa wapinzani wakubwa wakati Neymar alipokuwa Barcelona, lakini kwa sasa kila kitu kimebadilika baada ya Mbrazili huyo kuhamia PSG. Staa huyo wa Kibrazili ameanzisha nembo yake ya kibiashara inayofahamika kama INJR. Nembo hiyo imekuwa ikidhaminiwa na kampuni za maana kama Nike, Gillette na Red Bull. Kwa kupitia kampuni yake, Neymar amekuwa akihusisha na matukio mbalimbali ya uchangishaji pesa huko kwao Brazil. Mwaka 2016, alishirikiana na gwiji wa NBA, Michael Jordan katika kufanya biashara moja ya maana kuhusu viatu.
 
2.Cristiano Ronaldo- CR7 Brand

Supastaa wa Juventus, Cristiano Ronaldo kwa sasa ndiye mwanamichezo maarufu zaidi duniani. Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amelitengeneza jina lake na kuwa nembo ya kibiashara yenye nguvu zaidi. Nembo ya kibiashara ya staa huyo inayofahamika kama CR7 Brand imekuwa ikijihusisha na bidhaa kama pafyumu, viatu vya soka, hoteli, mavazi na vito. Staa huyo ameyahamishia mafanikio yake ya uwanjani kwenye biashara zake na mambo yanakwenda vizuri.
 
Back
Top Bottom