Gwiji la soka nchini Uingereza, Harry Redknapp amemfagilia nahodha wa Tottenhma, Harry Kane kwa kuwaongoza wenzake kuibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Wembley, wenyeji walifungwa bao la mapema na PSV dakika ya pili likiwekwa wavuni na De Jong, lililodumu hadi mapumziko.
Hata hivyo Kane mmoja wa washambuliaji mahiri wa Uingereza kwa sasa, aliirudisha Tottenham mchezoni alipofunga bao la kusawazisha dakika ya 78 kabla ya kufunga la ushindi dakika ya 89.
Redknapp, ambaye alipata kumnoa Kane kwa miaka mitatu wakati akiifundisha Spusr alisema mshambuliaji huyo amethibitisha ubora, thamani na umuhimu wake kama nahodha ndani ya kikosi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.