Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

446515639_442203~2.jpeg
 
Mwisho wa siku, nilifanikiwa kupata kila kitu nilichokihitaji. Mapenzi na heshima, ni vitu vya maana sana kwangu, zaidi ya mataji na tuzo. Nilijitolea kwa asilimia 101 kuwatumikia na kuwainua watu wangu,” Totti anasema katika moja ya mahojiano hivi karibuni.
 
Antonio Di Natale

“Hakuna mchezaji ninayemhusudu kutokana na misimamo wake pamoja uzalendo wake kama Di Natale,” aliwahi kuandika hivyo, Mwanahabari Daniel Storey katika moja ya makala zake kuhusu straika wa zamani wa Udinese, Antonio Di Natale. Licha ya ubora aliokuwa nao.
 
Antonio Di Natale anayetajwa kama mmoja kati ya washambuliaji ambao ulimwengu wa soka umepata kuwashuhudia, hakuyumbishwa na ofa kibao zilizokuja mbele yake. Aliendelea kuwa mwaminifu kwa klabu ya Udinese.
 
Tangu akiwa na miaka 25, mwaka alioanza kucheza soka la ushindani De Natale klabu kubwa kama Barcelona, AC Milan, Inter Milan, Man United na Real Madrid, zilikuwa zikihaha kuipata saini yake, yeye alikuwa anawaza kuipaisha Udinese. Akatundika daluga akiwa mfungaji bora wa miaka yote wa klabu hiyo.
 
Ulikuwa ni uamuzi mgumu, lakini nasikia faraja kuwa sehemu ya familia ya Udinese, Rais wa klabu na familia walinipenda na kunichukulia kama mwanafamilia, vitu vingine ni muhimu kuliko pesa,” alisema Di Natale akizungumzia maisha yake klabuni hapo.
 
Alan Shearer

Ni mmoja kati ya washambuliaji bora kuwahi kutokea katika soka la Kiingereza. Ndiye mfungaji bora wa muda wote Ligi Kuu ya England. Hata hivyo, mabao hayo ameyapatia katika klabu za Southampton, Blackburn na Newcastle United. Hakuwahi kukipiga timu kubwa. Timu ambayo ilitamani kumchukua ni Manchester United lakini iliambua patupu. Mara mbili alipata ofa ya kukipiga Man United ya Sir Alex Ferguson lakini alikataa.
 
Mara ya kwanza ilikuwa wakati akiwa na umri wa miaka 21 akiwa na Southampton ambapo alikataa na kwenda Blackburn. Mara ya pili ni pale wakati alipotaka kuondoka Blackburn na kutakiwa na Sir Alex lakini akajikuta akiishia katika klabu yake ya utotoni, Newcastle United.
 
Lakini haikuwa hivyo. Alichagua kwenda White Hart Lane na sio Old Trafford. Hii ilitokana na sababu za kimaslahi. Spurs ilikuwa tayari kuwajengea wazazi wake nyumba, huku pia ikiahidi kutoa ofa nyingine kwa ajili ya dada yake.
 
Bila kupepesa macho kiungo huyo akaitosa United. Akiwa White Hart Lane, Gascoigne alifanikiwa kujijengea jina na kuwa mmoja kati ya viungo hatari barani Ulaya wakati huo.

Katika fainali ya Kombe la Dunia, mwaka 1990, kwenye mchezo kati ya Italia na England, Gazza alionesha kiwango kikubwa. Hata hivyo, mpaka sasa watu wanajiuliza ingekuwaje kama angejiunga na United?
 
Jay-Jay Okocha

Kutoka Enugu hadi Istanbul, Paris na hatimaye Bolton Wanders. Bila shaka safari ya soka ya Jay-Jay Okocha, katika soka haikuwa rahisi.

Lakini pamoja na yote hayo, alichokifanya uwanjani kimebaki kuwa simulizi tamu katika midomo ya wapenda soka. Kiungo huyo mshambuliaji. Mwalimu wa Ronaldinho pale PSG. Mtu pekee ambaye Gaucho anamkubali mpaka leo, alikuja kuishangaza dunia akiwa chini ya mikono salama ya Sam Allardyce pale Uwanja wa Rebook .
 
Back
Top Bottom