Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Antonio Di Natale

“Hakuna mchezaji ninayemhusudu kutokana na misimamo wake pamoja uzalendo wake kama Di Natale,” aliwahi kuandika hivyo, Mwanahabari Daniel Storey katika moja ya makala zake kuhusu straika wa zamani wa Udinese, Antonio Di Natale. Licha ya ubora aliokuwa nao.
 
Antonio Di Natale anayetajwa kama mmoja kati ya washambuliaji ambao ulimwengu wa soka umepata kuwashuhudia, hakuyumbishwa na ofa kibao zilizokuja mbele yake. Aliendelea kuwa mwaminifu kwa klabu ya Udinese.
 
Tangu akiwa na miaka 25, mwaka alioanza kucheza soka la ushindani De Natale klabu kubwa kama Barcelona, AC Milan, Inter Milan, Man United na Real Madrid, zilikuwa zikihaha kuipata saini yake, yeye alikuwa anawaza kuipaisha Udinese. Akatundika daluga akiwa mfungaji bora wa miaka yote wa klabu hiyo.
 
Ulikuwa ni uamuzi mgumu, lakini nasikia faraja kuwa sehemu ya familia ya Udinese, Rais wa klabu na familia walinipenda na kunichukulia kama mwanafamilia, vitu vingine ni muhimu kuliko pesa,” alisema Di Natale akizungumzia maisha yake klabuni hapo.
 
Alan Shearer

Ni mmoja kati ya washambuliaji bora kuwahi kutokea katika soka la Kiingereza. Ndiye mfungaji bora wa muda wote Ligi Kuu ya England. Hata hivyo, mabao hayo ameyapatia katika klabu za Southampton, Blackburn na Newcastle United. Hakuwahi kukipiga timu kubwa. Timu ambayo ilitamani kumchukua ni Manchester United lakini iliambua patupu. Mara mbili alipata ofa ya kukipiga Man United ya Sir Alex Ferguson lakini alikataa.
 
Mara ya kwanza ilikuwa wakati akiwa na umri wa miaka 21 akiwa na Southampton ambapo alikataa na kwenda Blackburn. Mara ya pili ni pale wakati alipotaka kuondoka Blackburn na kutakiwa na Sir Alex lakini akajikuta akiishia katika klabu yake ya utotoni, Newcastle United.
 
Ahsante sana nijifunza kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…