Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezaji huyo amekuwa akipambana kupata namba katika kikosi hicho cha Old Trafford na pamoja na kuvuta pesa ndefu, amefunga mabao manne tu katika mechi 29.

Inarripotiwa kuwa Sanchez hana furaha United na mpango wake mzima ni kuondoka Old Trafford na ikiwezekana anataka ifikapo Januari dirisha dogo ltakapofunguliwa.
 
Mshambuluiaji huyo wa Chile pia amekuwa akitajwatajwa huko Paris Saint-Germain lakini iliwekwa sharti kwamba atachukuliwa ikiwa tu mchezaji mmojawapo kati ya Neymar au Kylian Mbappe wataondoka klabuni.

Lakini kwa mujibu wa televisheni ya Hispania, El Chiringuito, Sanchez amemwambia wakala wake, Fernando Felicevich kumtafutia timu.
 
Ripoti zinasema kuwa Felicevich alikuwa akihangaika na kuona uwezekano wa mteja wake kutua Santiago Bernabeu mapema Januari dirisha dogo litakapofunguliwa.

Mabingwa hao wa zamani Hispania wanahangaika kutengeneza safu ya ushambuliaji na ndio maana wamemsajili Mariano aweze kutua Lyon.
 
.MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck ameahidi atarudi kwa nguvu zote akiwa timu huku akiwashukuriu mashabiki wa klabu yake kwa kumpa nguvu kipindi hiki anachouguza enka yake aliyofanyiwa upasuaji.
 
Mchezaji huyo alianguka dakika ya 30 katika mchezo dhidi ya Sporting Lisbon ikiwa ni mfululizo wa michuano ya Europa League na kulazimika kuwekewa msaada wa hewa ya oksijeni, mpambano huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Emirates.
 
Arsenal ilithibitisha kuwa Welbeck anaendelea vizuri na kwamba anataraji atakuwa vizuri.

Welbeck hata hivyo, hatarajiwi kwa sasa kurudi msimu huu lakini matarajio ni kurudi upya baada ya kupona kabisa.
 
Mshambuliaji huyo aliwapongeza mashabiki wake kwa kumtumia ujumbe wa kutakia kila la kheri na akasema anawashukuru wote kwa kumuunga mkono na upendo.

‘Hakuna shaka nitakuwa vizuri na nitarudi mwenye nguvu zaidi. Naona mambo yanaanza sasa. Najua nitarudi nikiwa niko imara.’
 
Bernd Leno alisema kwamba kocha Unai Emery aliwaambia wachezaji wote wa Arsenal kwenda kumuona Welbeck kabla ya mchezo wa Arsenal na Wolves.

‘Nafikiri alifurahi sana kutuona. Welbeck ni sehemu ya timu na tutamsapoti kwa hali na mali,’ Leno alisema. ‘Ni suala la kuwa na subira na ukweli tunamkosa na Danny tunamuhitaji kwa ajili ya ushindi.
 
UKISIKIA kubwagamoyo ndiko huku, wakala wa kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil amesema ana ofa ya Chinese Super League itakayomwacha njiapanda kabla ya kusaini Arsenal.

Mapema Januari, Mjerumani huyo alikuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi Gunners’ akivuna Pauni £350,000 kwa wiki.
 
Lakini mwakilishi wa Ozil, Dr Erkut Sogut alisema kuwa mtu wake, moyo wake wote ameubwaga Arsenal, licha ya kupata ofa kibao kutoka nje ya Emirates.

‘Ukweli kuna ofa kibao Asia, Ni ofa za maana. Lakini kwa Mesut, pesa kwake si suala la kipaumbele, anachotaka yeye ni kucheza,’ Sogut aliliambia Evening Standard.
 
‘Pesa ni eneo moja muhimu la kuangalia, lakini watu wanatakiwa kuangalia, suala la soka ni kwa watu kujinasibu kwa kuangalia wapi unacheza.

"Soka la biashara ni muhimu kwa sasa. Kuna mambo ya kuangalia," alisema.

‘Mesut ni mchezaji mwenye wafuasi wengi klabuni, hata ukiangalia mauzo ya jezi yake, ni babu kubwa.
 
Mwisho wa siku, Haya yote tunakaa tunyaangalia na kuyafanyia kazi.

‘Kwa hiyo suala la soka biashara ni kitu muhimu kwa Mesut, amecheza timu nyingi na ameonyesha kiwango kiasi cha kuaminiwa na kupewa jezi namba 10 Ujerumani.

‘Soko lake ni dunia nzima. Klabu inpata pesa kutokana na viyu vyake mbalimbali, lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…