Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye Thierry Henry amepata ushindi wa kwanza tangu ateuliwa kuwa kocha wa Monaco baada ya kuilaza Caen 1-0.

Mfaransa huyo, aliyeitumikia Monaco kwa mafanikio makubwa alipewa kibarua cha kuinoa timu hiyo wiki sita zilizopita, lakini tangu ameanza kazi hiyo hakupata ushindi zaidi ya sare mbili na kupoteza nne.
 
Kabla ya kupewa kibarua hicho Henry, alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji na alitwaa mikoba hiyo baada ya klabu kumtimua Leonardo Jardim, katikati ya Oktoba ikiwa nafasi ya tatu kutoka chini.

Aidha huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Monaco kutofungwa bao tangu Agosti hata mechi ilizotoka sare ziliwa za mabao.
 
Nadhani Sarri anapaswa kuangalia mpango mwingine, kwa sasa amefeli, bila shaka kumtumia N’Golo Kante kama beki namba nne sio sahihi, vizuri ampumzishe kuliko kumchezesha namba isiyo yake ili kumpisha Jorginho,” alisema.
 
Katika mchezo dhidi ya Spurs uliochezwa Wembley, Chelsea ilifungwa mabao 3-1 na Desailly aliyeitumikia timu hiyo katika michezo 158 na kufunga mabao sita, alisema kinachoigharimu timu hiyo ni kujilinda zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…