Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2.Alan Shearer- mabao 5 vs Sheffield (1999)

Staa wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer alifunga mabao matano katika mechi moja wakati timu yake hiyo ilipoichapa Sheffield Wednesday 8-0, Septemba 1999. Fowadi huyo matata kabisa alikuwa akifunga mabao kama anavyotaka kwa kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi hicho cha St. James Park na kile cha Blackburn Rovers. Anashikilia rekodi ya mabao kwenye ligi, akifunga mara 260.
 
1.Andy Cole- mabao 5 vs Ipswich (1995)

Gwiji wa Manchester United, Andy Cole alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England. Staa huyo wa zamani wa England alifunga mara tano wakati Man United ilipoichapa 9-0 Ipswich Town mwaka 1995. Msimu huo alimaliza akifunga mabao 12 katika mechi 18 alizocheza kwenye ligi. Alitua Man United kwenye dirisha la Januari akitokea Newcastle United.
 
Chini ya Kocha wao mpya, Unai Emery, Arsenal walianza vibaya Ligi Kuu ya England (EPL) kwa kufungwa mechi mbili mfululizo, lakini tangu hapo wamekuwa ni mwendo wa ushindi na sare, kote EPL, Ligi ya Europa na Kombe la Ligi.
 
Emery anasema hana cha kuchagua, bali anatia nguvu kote, akiwa na nia ya kutwaa taji lolote litakalokuwa njiani mwake, hivyo anazungusha kikosi chake kuendana na matakwa ya nyakati, yaani kuwatazama wapinzani wao wakoje.
 
Tulimwona akiwa benchi pamoja na Aaron Ramsey kwenye mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Bournemouth kwenye Uwanja wa Vitality na kocha huyu haoni tabu, kwani amekuwa hata akiwatoa nyota hao uwanjani na kuwarudisha benchi anapoamua.
 
Je, Washika Bunduki wa London watakabiliana na Spurs walio moto, wakitoka kuwapiga Chelsea 3-1 wikiendi iliyopita wakitumia mfumo gani? Je, Emery atatumia 3-4-3 walioutumia kuwafunga Bournemouth? Ipi nafasi ya Ozil? Emery amekuwa tofauti kabisa na mwenzake wa Chelsea, Maurizio Sarri anayeshikamana na mfumo wake wa 4-3-3.
 
Ozil - mchezaji wa kimataifa mstaafu wa Ujerumani, ametengeneza nafasi 20 kwenye EPL msimu huu, nyingi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Arsenal. Amecheza dakika 825 kwenye mechi za daraja la juu msimu huu kati ya dakika 1,170.
 
Ametengeneza nafasi hizo katika wastani wa kila dakika 41.25, akishika nafasi ya 16 kati ya wachezaji wote na katika misimu yote aliyokaa Arsenal, amemaliza katika nafasi tano za juu.

Misimu miwili akishika nafasi ya k,wanza kwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi.
 
Ozil ni mchezaji namba 10 bora zaidi wa Arsenal lakini ikiwa Emery ataendelea na mfumo huo, basi hakuna namba 10 na kwa msingi huo Ozil hatacheza, labda awekwe kwenye nafasi nyingine, maana hata Jumapili alibaki amejikunyata kwenye benchi hadi mechi kumalizika.
 
Emery alipoulizwa kulikoni Ozil hakucheza, alijibu ni kwa sababu alikuwa akitarajia mechi ngumu inayotaka misuli na shuruba sana na kasi.

Ozil hajacheza tangu watoke sare na Wolves Novemba 11, sasa huwezi kusema amechoka. Pengine Emery amemchoka.
 
Wala haidhaniwi alipumzishwa kwa ajili ya kuwa tayari kwa safari na mechi ya Alhamisi dhidi ya Vorskla Poltava, kwa sababu hajapata kuanza dakika ya kwanza ya mechi yoyote ya Europa na zaidi ya hayo The Gunners wameshajihakikishia kusonga mbele Kundi E.

Kwa msingi huo, ningekuwa mie ni Ozil, nisingekuwa na raha, maana kila kitu kinaonekana kuwa dhidi yangu; kocha akisema eti mchezaji mzoefu kama huyo hangeweza kucheza kwenye mechi ngumu, ina maana anamwona ni ‘mayai’.
 
Tukiwa ndani ya miezi minne tu katika msimu huu, bila shaka yapo makubwa na mengi mbeleni ya kusubiri, kutazama na kusikia na wachezaji wenye majina madogo wanapewa nafasi huku kina Ramsey na Ozil wakisota benchi.

Kocha huyu amekuwa tofauti kabisa na mtangulizi wake, Arsene Wenger, aliyekuwa akimtumia sana Ozil na Ramsey.
 
Back
Top Bottom