Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini...
 
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama; JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii? LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi JAMAA AKAZIMIA HAPOHAPO
 
USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA. Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika nyumbani. kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao. Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi, akawaambia "hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani" mama"hee embu tuoneshe mwanangu" jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu "ngapi?" wazazi"moja" akainua wa pili "ngapi?" wazazi "mbili" akawarudisha akisema"wazee wangu nadhani japo shule hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu mezani" baba"mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA
 
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa. RAFIKI: Nini tena? JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje? JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’
 
Marafiki wawili*(Elias na Ben)* walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu. Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo: *Ben:* Muone yule mrembo amenirushia busu *Elias:* tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali.. _(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)_ *Ben:* yule mwanamke ameniita! *Elias:* Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha. *Ben:* Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu *Elias:* Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule _(akihisi kutotiliwa maanani)_ _(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini)_ .. 🔊🔊 *Lady:* _(akiangalia kupitia dirishani)_ Oooh! Yule ni mume wangu!! *Ben:* Mama yangu ! Nipo matatani, kweli ? ..!! *Lady:* Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo (akimuonyesha lundo la nguo) _(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)_ _(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)_ *Ben:* Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano??? *Elias:* Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, *Nilizifua Mimi Juzi!!* 😂😂😂😂😂😂😂😂😂 *When an experienced person speaks ... 👂you must listen..!*
 
Wadada wa siku hizi wanaona bora kumuachia House girl mtoto mdogo anayenyonya,ye akaenda kazini na moyo ukawa na amani kabisa. Kuliko kumuacha House girl huyo huyo na Mume,hata akisafiri kwa siku Mbili. 😂😂i😂😂🙌🏻🙌🏻🙌🏻
 
Mtumishi wa MUNGU mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police,police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi, mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? mbona gari lako matairi yameisha, hatimaye polisi akamuamuru padre waende nae kituoni. Njiani polisi alimuuliza , umesema wewe ni Mtumishi wa MUNGU, je unabiblia ndani ya gari, akajibu ndio ninayo, polisi akamuambia , pack ...gari pembeni na unipe biblia. Mtumishi akapaki gari na kumpa biblia yule polisi,Polisi akasita kupokea, akamwambia Mtumishi 'fungua na usome Mathayo 5:25-26 "Mtu wa Mungu akasoma ": "Patana na Mshtaki wako upesi,wakati uwapo pamoja naye njiani: yule mshtaki asijekukupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari,ukatupwa gerezani. " Amin nakuambia,Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho" Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu".. Enenda kwa amani
 
Bibi alienda kupiga Xray, Doctor akamwambia moyo umetoboka katikati na pembeni umevimba pande mbili. Bibi akasema we mtoto wewe nadhani umechanganya negative ya picha ya mtu alipiga matako yake? Nenda kalete ya kwangu
 
Mzee mmoja aliwakataza vijana kuvuta bangi karibu na nyumba yake,Wavuta bangi wakaamua kumwamisha huyo mzee nanyumba yake,kwanza wakavuta bangi ya kutosha wakavua mashati wakaanza kusukuma ile nyumba, kibaka akapitia yale mashati, mmoja wao alivyogeuka nyuma hakuyaona akajua wameshafika mbali akawaambia wenzie tukazane tumefika mbali hata nguo zetu hazionekani wakaendelea mpaka bange zilivyoyeyuka kchwani wakaona wako palepale.
 
Back
Top Bottom