Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_20181201_202405.jpeg
 
WATU wanatetemeka wakati Michael Owen alishabeti zamani kuhusu mechi ya kesho Jumapili ya watani wa jadi wa London Kaskazini, Arsenal dhidi ya Tottenham katika pambano ambalo litachezwa pale Emirates nyumbani kwa The Gunners.
 
Owen, staa wa zamani wa Liverpool, Real Madrid, Manchester United na Timu ya Taifa ya England amedai baada ya kuchungulia sana amegundua pambano hilo litamalizika kwa sare yenye mabao na unaweza kumsikiliza.
 
Arsenal haijafungwa katika mechi 11 za Ligi Kuu ya England tangu ilipofungwa na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu na imeshinda mechi nane huku ikitoka sare tatu kuashiria mwanzo mpya wa timu hiyo chini ya Kocha wa Kihispaniola, Unai Emery.
 
Wapinzani wa London Kaskazini Arsenal dhidi ya Spurs unaweza kutegemea itakuwa mechi ya kuburudisha wakati wanapambana. Itakuwa mechi kali Jumapili. Arsenal itakuwa na presha ya kushinda kwa ajili ya kupunguza pengo lao hadi pointi tatu na mbio za kumaliza nafasi nne za juu ni wazi kutakuwa na timu tatu za London (Arsenal, Chelsea na Tottenham),” alisema Owen.
 
Back
Top Bottom