Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alifanikiwa kufikia boya na akaanza kulielekeza kama ngalawa akitumia mikono yake kama makasia kutoroka visiwa vilivyokuwa mikononi mwa Wajapani.
Alikuwa na bahati ajabu, kwani kabla hajakwenda mbali nyambizi iliibuka alikokuwa na kumwokoa. Nyambizi hiyo iliendesha shughuli zake kwa utaratibu sana hivi kwamba walirekodi kwa filamu.
 
Baada ya kuondoka kwenye kikosi cha wanamaji mwaka 1945 kwa heshima, Bush alimwoa msichana mwenye umri wa miaka 18, Barbara Pearce.
Ndoa yao ilidumu miaka 72 na wakafanikiwa kuwapata watoto sita.
Mwana wao wa kwanza, ambaye baadaye alikuwa Rais George Walker Bush, alizaliwa mwaka mmoja baadaye.
 
Awali Bush alikuwa amepewa nafasi kuendelea na elimu katika Chuo Kikuu cha Yale kabla ya kusajiliwa katika kikosi cha wanamaji. Mara tu alipotoka jeshini mwaka 1945 baada ya vita kumalizika, alirudi katika chuo Kikuu na kukamilisha shahada yake katika sanaa.
 
Busha na familia yake kisha walihamia Texas ambako alitumia uhusiano mzuri wa kibiashara wa baba yake kupata kazi katika sekta ya mafuta.
Kabla ya kufikisha miaka 40, tayari alikuwa milionea.
Bush na mkewe Barbara walisononeka sana baada ya binti yao wa pekee kugunduliwa kuwa na maradhi ya kansa ya kukosekana kwa damu mwilini, kwa Kiingereza Laukaemia. Robin alipelekwa hospitalini kutokana na uchovu mwilini lakini Bush na mkewe walishtushwa na maelezo ya daktari.
 
Familia hiyo ilishtushwa na kifo cha Robin miezi michache baadaye.
Pigo la tukio hilo lilijitokeza baada ya kifo cha
Barbara Bush alipofariki miaka 65 baadaye, familia hiyo iliweka bango lenye maandishi yaliyosema "Tafadhali mama, mkumbatie Robin kwa niaba yetu.
 
Uhafidhina
Mawazo ya kikazi ya George Bush yalibadilika na kuingilia siasa.
Baada ya kuhudumu kwa muda kama mwenyekiti wa tawi la chama cha Republican eneo la Texas, alifanya uamuzi mgumu. Alishindana kutaka kuteuliwa kama mgombea wa Useneta wa chama chake cha Republican katika jimbo la Texas.
Seneta wa eneo hilo wa chama cha Democratic aliwaambia watu kuwa Bush alikuwa mwanasiasa wa msimamo mkali wa mrengo wa kulia.
 
Mwanachama huyo wa Democtatic alipata asilimia 56 ya kura zilizopigwa zikilinganisha na asilimia 43 za Bush. Bila kukata tamaa Bush aligombea kiti cha bunge la wawakilishi na akashinda kiti mwaka 1966. Alihudumu mihula mbili.
Rais Richard Nixon alimshawishi Bush kugombea Useneta tena mwaka 1970 lakini tena akashindwa na mgombea yule yule wa Democratic.
Rais Nixon alimteua Bush kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa 1971 na kisha akawa mwenyekiti wa chama cha Republican.
 
Wakati Nixon alipolazimishwa kujizulu 1974, Bush alifanya kila juhudi kuponyai baadhi ya makovu yaliyosababishwa na kashfa ya Watergate, ambapo alitumia muda wake mwingi kuwatetea wagombezi wa Republican kwa kufanya ziara maeneo mbalimbali nchini humo.
Mwisho wa mwaka alienda Uchina kuwa balozi katika ubalozi mpya wa Marekani nchini humo.
 
Baada ya kuwa nchini Uchina kwa mwaka mmoja pekee, Rais Gerald Ford alimrejesha nyumbani Bush na kumteua kuwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la CIA, shirika ambalo lilikuwa limekabiliwa na msururu wa kashfa kuhusiana na operesheni za usiri mkubwa nje ya nchi pamoja na kuwapeleleza raia wa Marekani bila idhini.
Kuutmwa kwake CIA kulitokea wakati ambapo mkewe Barbara alikuwa amezidiwa na ugonjwa wa kiakili.
 
Mke wake aliandika kwenye kitabu kuhusu maisha yake kwamba angelielekeza gari lake pembeni mwa barabara akiogopa kugonga mti au magari yaliyokuwa yakienda upande ule mwingine. Hisia hizo baadaye zilitokomea.
Bush aliondoka CIA baada ya Ford kuondoka madarakani na mwaka 1978 akaanza kufanya kampeni ya kutaka kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama chake katika uchaguzi wa mwaka 1980.
 
Alizuru kote nchini akieleza juu ya msimamo wake wa uhafidhina wa kadri. Kufikia 1980 ilionekana wazi kuwa ni yeye pekee aliyebakia ambaye angetoa ushindani mkali dhidi ya Ronald Reagan.
Mara tu alipojiingiza katika kinyang'anyiro cha kisiasa, Bush aligundua kuwa kulelewa kwake katika maisha ya hadhi awali kungekuwa kama gharama kwake kisiasa.
"Kuna kosa gani katika kufaulu maishani, " Bush aliuliza wakati ule. Aliongezea :" Kuna kosa gani kuwa na elimu nzuri? Kuna kosa gani ikiwa nilifaulu maishani na katika biashara zangu au kuwa balozi mzuri nchini Uchina au katika Umoja wa Mataifa au kufanya kazi nzuri katika CIA. Haya yote nimefanya mimi. Najua wengine watasema ni kujigamba lakini hiyo ndiyo rekodi yangu."
 
Aliposhindwa na Reagan alikuwa na bahati nyingine ya kumliwaza. Aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa reagan ambapo alihudumu kama makamu wa Rais kwa miaka minane, ambapo ilikuwa ni kama kipindi cha mafunzo ya kujiandaa kuwa Rais.
 
Soma midomo yangu
Katika uchaguzi wa 1988 ambapo alishinda na kuwa Rais, George H W Bush alifanya makosa mawili makubwa.
Kosa la kwanza ni kumchagua Makamu wa Rais asiyejulikana: Dan Quayle, aliyekuwa Seneta wa hadhi ya chini kutoka Indiana. Quayle alijulikana kimataifa zaidi kutokana na makosa aliyoyafanya kwenye hotuba na mazungumzo yake.
 
Kosa la pili lilikuwa kuahidi wakati wa kampeni kuwa hataongeza kodi wakati wa Kongamano kuu la chama cha Republican la kuidhinisha mgombea urais mwaka 1988..
Alipokuwa anamshambulia na mpinzani wake wa chama cha Democratic Michael Dukakis kuhusu sera yake ya kifedha, alitoa ahadi hiyo ambayo baadaye ilichangia kumuondoa madarakani.
'Isomeni midomo yangu,' aliwaambia wajumbe waliokusanyika. 'Hakuna kodi mpya.'
 
Baada ya kampeni kali sana kuwahi kufanyika nchini humo, Bush alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais tangu kuchaguliwa kwa Martin Van Buren kuwa rais mwaka 1836.
Wakati huu ulikuwa wa kipekee kwa sababu hapo ndipo Serikali ya Muungano ya Usovieti uliporomoka na 'Ukuta wa Chuma' uliodaiwa kutenganisha Ulaya Mashariki na Ulaya Magharibi 'ukabomoka'.
 
George H W Bush aliingia madarakani wakati wa mabadiliko makubwa katika siasa za dunia. "Upepo mpya unavuma, na dunia iliyotiwa upya matumaini na uhuru inaonekana kuzaliwa; kwani ndani ya moyo wa binadamu, kama si kwa kweli kabisa katika uhalisia, enzi ya dikteta imefikia kikomo," alitangaza akiwa kwenye vidato vya jengo la Capitol
"Upepo mpya unavuma, na dunia iliyotiwa upya matumaini na uhuru inaonekana kuzaliwa; kwani ndani ya moyo wa binadamu, kama si kwa kweli kabisa katika uhalisia, enzi ya dikteta imefikia kikomo," alitangaza akiwa kwenye vidato vya jengo la Capitol, makao makuu ya bunge la Congress.
 
Msiyumbeyumbe, George
Mtihani mkubwa kwa Bush ulilijitokeza wakati Iraq iliposhambulia Kuwait kwa ghfula Agosti 1990.
Bush aliunda muungano wa kijeshi wa kimataifa kushambulia Iraq nchini Kuwait kuhakikisha majeshi ya Saddam Hussein yanatimuliwa huko.
Wakati huo huo alanzisha kikosi maalumu cha wanajeshi wa Marekani kupiga kambi nchini Saudi Arabia, eneo zuri kuweka wanajeshi wa kukabiliana na maadui wa Marekani katika Ghuba.
 
Iraq ilipoishmabulia Kuwait mwaka 1990, George H W Bush alikabiliwa na mtihani mkubwa zaidi katika sera ya kigeni. Alipoamua kuchelewesha hatua ya kijeshi ili kupata idhini kutoka kwa Umoja wa Mataifa, Margaret Thatcher anakumbukwa kwa kumtahadharisha kwamba 'huu sio wakati wa kuyumbayumba'.
Busha alichelewesha kushambulia Iraq nchini Kuwait kwa sababu alikuwa akisubiri kupata idhini ya Umoja wa Mataifa. Lakini alishutumiwa vikali na aliyekuwa Waziri Mkuu Uingereza Margaret Thatcher.
"Ni sawa George lakini huu si wakati wa kuyumbayumba," ndivyo alivosema Bi Thatcher katika simu aliyompigia Bush usiku wa manane kutoka Downing Street.
Vita vilivyofuata viligeuka kuwa ushindi mkubwa kwa Marekani na wataalamu wa kijeshi wa Marekani walipongezwa na taifa kwa jumla lilifurahia hadhi iliyotokea kwa jeshi baada ya mapigano hayo.
Chini ya uongozi wa Marekani mapigano hayo yaliendelea kwa saa 100 pekee.
 
Vita vya Ghuba vya 1991 vilikuwa moja ya mtihani mkubwa zaidi kwa uongozi wa Bush. Vita vya ardhini vilidumu saa 100 pekee lakini Saddam Hussein hakuondolewa madarakani
Ushindi huo uliimarisha hadhi aliyokuwa nayo Rais Bush licha ya kwamba kikosi hicho cha muungano hakikuingia Baghdad kwenyewe ambapo kilimwacha Saddam Hussein kuendelea kuwa mamlakani.
Kumpindua Saddam Hussein na serikali yake kulitekelezwa na mwanawe Bush baadaye.
 
Vita vya Ghuba vya 1991 vilikuwa moja ya mtihani mkubwa zaidi kwa uongozi wa Bush. Vita vya ardhini vilidumu saa 100 pekee lakini Saddam Hussein hakuondolewa madarakani
Ushindi huo uliimarisha hadhi aliyokuwa nayo Rais Bush licha ya kwamba kikosi hicho cha muungano hakikuingia Baghdad kwenyewe ambapo kilimwacha Saddam Hussein kuendelea kuwa mamlakani.
Kumpindua Saddam Hussein na serikali yake kulitekelezwa na mwanawe Bush baadaye.
 
Back
Top Bottom