Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Ingawa umaarufu wake ulipanda na kufikia asilimia 90 wakati mmoja, uamuzi wa Bush wa kutilia mkazo masuala ya nje ya nchi kulifanya wakosoaji wake wengi kusema kuwa alikuwa akipuuza masuala ya nyumbani na kusababisha maisha kuwa magumu sana kiuchumi tangu vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Alishinikizwa sana na wanachama wa Democratic ambao walidhibiti bunge, lakini Bush alisisitiza kwamba makali ya mgogoro wa kiuchumi wa wakati huo yalikuwa yamepita.
"Tutaliondoa taifa hili kutoka katika ugumu wa kiuchumi," Bush aliahidi. "Hatua kwa hatua na wale wanaotaka kutuchelewesha au kutuzua bora watuondokee njiani."