Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Robert Lewandowski- Bayern Munich

Fowadi supastaa wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ni mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa duniani kwa sasa.

Kwa mujibu wa vigezo vya ESPN, kwa kuzingatia mambo yao waliyozingatia, Lewandowski imemweka kwenye namba tano. Msimu huu, fowadi huyo wa kimataifa wa Poland amefunga mabao 22 katika mechi 22 alizoitumikia klabu hiyo.

Msimu uliopita alifunga mabao 41 katika mechi 48. Kwa maana hiyo kwa mabao yake aliyofunga kwenye kikosi hicho cha Allianz Arena, Lewandowski amefunga mabao 173 katika mechi 217.
 
4. Luis Suarez- Barcelona

Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez hadi sasa msimu huu ameshatikisa nyavu mara 11 katika mechi 20 alizochezea timu hiyo ya Nou Camp.

Jambo hilo linamfanya awe amefikisha mabao 163 katika mechi zake 218 alizochezea klabu hiyo vijana wa La Liga kwa msimu huu. Hakika hiyo ni rekodi vora kabisa. Msimu uliopita alifunga mabao 31 katika mechi 51 za michuano yote aliyoitumikia Barcelona.

Suarez ametengeneza kombinesheni matata kabisa na Lionel Messi tangu Mbrazili Neymar alipoondoka kwenye kikosi hicho kwenda kujiunga na Paris Saint-Germain.
 
3. Edinson Cavani- PSG

Fowadi wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani ameonekana kuwa hatari zaidi kuliko washirika wake Neymar na Kylian Mbappe. Fowadi huyo wa kimataifa wa Uruguay amefunga mabao 12 katika mechi 16 alizocheza hadi sasa msimu huu.

Msimu uliopita alifunga mabao 40 katika mechi 47. Kwa maana hiyo, hadi sasa kwa kipindi chote alichocheza kwenye timu hiyo ya Ligi Kuu Ufaransa, amefunga mabao 182 katika mechi 261.

Cavani ni mmoja kati ya washambuliaji matata kabisa duniani ambao suala la kufunga halijawahi kuwa tatizo kwa upande wao.
 
2.Sergio Aguero- Man City

Kinara wa mabao wa muda wote klabuni Manchester City, Sergio Aguero amepangwa namba mbili kwenye chati za ESPN. Fowadi huyo wa Kiargentina amefunga mabao 211 katika mechi 309. Msimu huu mambo yake yamekuwa magumu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini bado ameweza kufunga mabao 12 katika mechi . Msimu uliopita, alifunga mabao 30 katika mechi 39.

Kocha Pep Guardiola alijaribu kumweka nje ya kikosi chake, lakini aligundua kwamba straika huyo hana mbadala kwenye kikosi hicho cha Etihad.
 
1.Harry Kane- Tottenham

ESPN imemchagua Harry Kane kuwa ndiye straika namba moja kwenye viwango vyao kwa mwaka huu.

Fowadi huyo wa Tottenham Hotspur amefunga mabao 13 katika mechi 23 alizocheza msimu huu.

Msimu uliopita aliweka mipira kwenye nyavu mara 41 katika mechi 48 na msimu wa 2016/17 alifunga mabao 35 katika mechi 38.

Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika huko Russia alifunga mabao sita na kuifikisha England nusu fainali huku akishinda Kiatu cha Dhahabu katika fainali hizo. Straika Kane ni supastaa wa kutegemewa huko kwenye kikosi cha Tottenham.
 
Kocha huyo Mreno aliiacha familia yake huko kwenye Jiji la London, alikopanga nyumba yenye thamani ya Pauni 25 milioni katika kitongoji za Belgravia, ambako binti yake, Matilde na mtoto wake wa kiume Jose Jr wanaishi pamoja na mama yao.
 
Yeye Mourinho kwa muda wote, tangu alipochukua kibarua cha kuinoa Man United katika majira ya kiangazi mwaka 2016, amekuwa akiishi katika hoteli maarufu ya nyota tano ya Lowry iliyopo kwenye Jiji la Manchester.

Hadi anafutwa kazi, Mourinho alikuwa akiishi kwenye hoteli hiyo, akitumia siku 895 na kumgharimu kiasi cha Pauni 779,000.
 
Familia ya Mourinho inaishi London, ambapo binti yake anasoma katika Chuo Kikuu cha Sanaa cha London na mtoto wake wa kiume alikuwa anachezea Fulham hadi kufikia Aprili mwaka jana.

Mourinho amesema watoto wake wapo kwenye umri ambao hawawezi kuandamana naye kila mahali anapokwenda, wanahitaji kutulia sehemu moja na kufanya mambo yao.
 
Kuepuka kuwa na makazi mengine kwenye Jiji la Manchester, Mourinho aliamua kuishi kwenye hoteli hiyo, ambayo ndio hasa inayotumiwa na timu ya Man United inapojiandaa na mechi zake za nyumbani. Hata hivyo, makazi hayo ya hotelini, yamemgharimu Mourinho Pauni 779,000 ikiwa ni zaidi ya mara tatu ya pesa ambazo angelipa kama angeamua kupangisha nyuma ya kawaida tu, ambayo gharama yake ingekuwa Pauni 240,000.
 
Mara kadhaa mashabiki wa Man United wamemtaka kocha huyo atafute makazi yatakayomfanya kutuliza akili yake na kuisaidia timu, lakini mwenyewe alisema hapo kwenye hoteli ndipo panapomfanya awe huru.

Chumba chake alichokuwa akiishi Mourinho hotelini hapo kiliitwa The Riverside, ambapo kwa usiku mmoja gharama yake ni Pauni 870.
 
Kwa maana hiyo, kwa siku 895 Mourinho alizoishi kwenye hoteli hiyo, kila siku alikuwa akilipa Pauni 870, hivyo ni karibu Pauni 779,000 zimemtoka kwenye kugharimia makazi yake tu kwa muda wake aliokuwa kwenye kiti chake cha ukocha kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
 
Chanzo cha habari kimoja kilifichua hili: “Kuna mambo yalikuwa yakiendelea baina ya Mourinho na kikosi, lakini hajawahi kuwa na shida kwenye sehemu ya kuishi. Alikuwa na furaha The Lowry – licha ya kwamba hakufurahia kuwa mbali na familia yake. Kubwa zaidi alifurahia mpangilio wa makazi yake ulivyokuwa.”
 
Chumba alichokuwa akiishi Mourinho kulikuwa na kila kitu, ikiwamo baa ndogo ambayo alikuwa akiitumia kocha huyo kuburudika na vinywaji anapokuwa na wageni.

Kitanda chake ni cha kifalme na hata bafu ni kubwa la kujiachia. Kuna mgahawa pia wa kisasa kabisa, huku mnofu wa nyama ukigharimu Pauni 32. Wachezaji wa Man United wamekuwa wakipelekwa hotelini hapo kila siku ya mchezo ili kutuliza akili zao na kutosumbuliwa chochote. Kwenye Hoteli ya Lowry kuna ulinzi wa kutosha muda wote na klabu ya Man United inapohitaji ulinzi uimarishwe zaidi basi jambo hilo hufanyika mara moja.
 
Mwaka 2015, kipindi hicho Man United ilipokuwa chini ya Kocha Louis Van Gaal, walinzi walipelekwa hotelini hapo kuyafanyia upekuzi mabegi yote kabla ya kikosi cha timu hiyo kupata mlo wa usiku. Mwaka jana walinzi hao walikuja kuilinda Man United kwa mbwa kabla ya mechi baina ya timu hiyo dhidi ya Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…