Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Morata amekuwa na wakati mgumu kupata namba ya mara kwa mara Chelsea chini ya kocha wake Maurizio Sarri na hakupangwa kwenye mmechi tatu za mwisho za timu hiyo.

Wakati Morata hakupangwa siku hizo, Higuain hajafunga bao tangu Oktoba.

Kwa mujibu wa Sport Mediaset, kila upande umekubali kimsingi kumwachia mchezaji wake.
 
Hata hivyo, Higuain anaichezea AC Milan kwa mkopo akitokea Juventus, hivyo klabu hiyo itataka uthibitisho wa Juventus, na mabosi wa klabu hiyo wanaamini kuwa mechi zijazo za Frosinone na SPAL zitakuwa za mwisho kwake.

Naye Morata anataka kurudi Italia baada ya kukosa nafasi Chelsea na Sarri alimuuliza kuhusu Higuain na kusema ni mchezaji mzuri.
 
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, amesema anaamini wachezaji wengi watang’oka kwenye klabu hiyo kwa sasa kutokana na mabadiliko ya benchi la ufundi.

Essien ameyasema hayo baada ya beki chipukizi kutoka Denmark, Andreas Christensen, kuomba kuondoka akiamini mchango wake hauhitajiwi na kocha Maurizio Sarri.
 
Alisema anajua watakaoondoka ni wengi miongoni mwao ni mshambuliaji Alvaro Morata, Cesc Fabregas, Ruben Loftus-Cheek, Gary Cahill, Danny Drinkwater, Victor Moses na chipukizi Callum Hudson-Odoi.

“Kila mchezaji anatamani kucheza na pale unapokosa nafasi unachanganyikiwa, pale Stamford Bridge ni pagumu sana kupata nafasi ya kucheza kila mechi tena ikitokea ukakumbwa na majeruhi,” alisema Essien.
 
Kiungo huyo aliyeweka rekodi ya ada alipotua Chelsea mwaka 2005 akitokea Lyon ya Ufaransa akiwa muafrika kwa kwanza kusajiliwa kwa fedha nyingi aliigharimu Pauni 24.5 milioni.

Alicheza kwa misimu tisa na kutwaa mataji mbali mbali yakiwemo mawili ya Ligi Kuu England, Kombe la Ligi, manne ya FA, mawili ya Ngao ya Jamii na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…