Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wenger amekuwa akikosolewa kwa kuwa na timu zenye safu mbovu za mabeki, lakini vikosi vyake vote alivyowahi kuvitengeneza kwa miaka yake 22 kwenye klabu hiyo, hakuna hata kimoja kilichozidiwa na kufungwa mabao mengi kuliko hiki cha Emery.
 
Emery anahitaji kusajili beki mwingine kwenye dirisha la Januari.

Mwezi huu, imeruhusu mabao 14, hiyo ni kwenye mechi saba tu. Achana na yale mabao mawili iliyofungwa na Tottenham Hotspur kwenye Kombe la Ligi. Ina beki mbovu hakika na Emery haonekani kufahamu kitu gani cha kufanya kunusuru mambo.
 
Alibadili baadhi ya vitu baada ya kutua Arsenal. Alibadili hata mfumo na kuifanya timu icheze anavyotaka yeye. Lakini ameshindwa kufanya kitu muhimu kwenye kuzima matobo yaliyopo kwenye safu yake ya mabeki.

Ubovu wa beki si tu umeumbuliwa na timu vigogo kwenye EPL, bali imeruhusu wavu wake kuguswa na timu za kawaida kabisa kama Burnley, Brighton na Southampton.
 
Kwenye Boxing Day, Alex Iwobi alinaswa na kamera za uwanjani akimuuliza mwenzake fomesheni gani wanacheza walipokuwa wakimenyana na Brighton. Hilo linatosha kuthibitisha kuwa Unai Emery anawavuruga wachezaji wake na ndio maana na yeye wanamvuruga katika matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…