3.Juventus - Euro 256.9 milioni
Juventus imetumia pesa nyingi sana kwenye dirisha la majira ya kiangazi, ambapo walitoa mkwanja mrefu kwenye usajili wa supastaa wa Ureno, Cristiano Ronaldo waliyemnasa kutoka Real Madrid. Kwenye usajili wa staa huyo, zaidi ya Euro 100 milioni zilitumika, kisha wakamnunua kumrudisha kwenye kikosi chao beki wa kati, Leonardo Bonucci. Waliwanunua jumla pia mastaa kama Douglas Costa na Joao Cancelo kuwaongeza kwenye kikosi chao na hivyo kuwafanya kutumia pesa nyingi sana kwenye dirisha hilo la majira ya kiangazi wakishika namba tatu katika timu iliyotumia mkwanja mrefu kwenye usajili kwa mwaka 2018, wakitumia Euro 256.9 milioni.