Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kinara huyo wa mabao huko Arsenal, akiwa amefunga mara 13 kwenye Ligi Kuu England hadi sasa msimu huu, alitolewa katika dakika 20 za mwisho na nafasi yake kuingia straika wa Kifaransa, Alexandre Lacazette.
 
Kwenye mechi hiyo, Kocha Unai Emery aliamua kutowaanzisha pamoja washambuliaji wake hao akiamua kuachana na mfumo wa 4-1-2-1-2 (diamond) kutokana na timu kuwa na shida kwenye safu ya mabeki. Arsenal ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa Ainsley Maitland-Niles, lakini baada ya hapo yenyewe ndio iliyokuwa ikiokota tu mipira kwenye nyavu zake na kuja kuanza kati, ambapo Roberto Firmino alipiga ‘hat-trick’, Sadio Mane akapiga moja na Mohamed Salah akapiga jingine.​
 
Man United kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda, Ole Gunnar Solskjaer aliyechukua majukumu ya kuinoa timu hiyo baada ya kufutwa kazi kwa Jose Mourinho, lakini ni jambo linalofahamika wazi Mashetani Wekundu wanatafuta kocha mpya mwishoni mwa msimu.
 
Bado nina mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wangu hapa Juventus. Nipo vizuri sana mahali hapa na mambo yanakwenda poa. Ndio kwanza Desemba, hivyo acha tusubiri kwa sababu kutoka sasa hadi Juni kuna mechi nyingi sana hapo kati,” alisema.
 
Klabu nyingi sana za Ulaya zilifanya usajili wa pesa ndefu kusainisha wachezaji wapya ili kuboresha vikosi vyao kuweza kutamba kwenye michuano mbalimbali. Kwenye suala hilo, hakika kuna timu zilifanya usajili wa pesa nyingi sana.
Hizi hapa ndio klabu tano zilizotumia pesa nyingi kwenye usajili kwa mwaka huu wa 2018.
 
5.PSG - Euro 177 milioni
Paris Saint-Germain walishakuwa wamekubaliana na AS Monaco kumbeba jumla staa wao Kylian Mbappe baada ya kucheza kwenye kikosi chao kwa mkopo msimu mzima. Dili hilo lilikamilishwa kwenye majira ya kiangazi mwaka huu huko Ulaya na hakika Mbappe alibebwa kwa pesa nyingi sana. Kisha PSG iliwaongeza mastaa Thilo Kehrer na Juan Bernat kwenye kikosi chao na kuwafanya wawe wametumia kiasi cha Euro 177 milioni kwenye usajili na kuwa timu namba tano ya Ulaya ilitumia mkwanja mrefu kwenye kufanya usajili wa wachezaji kwa mwaka huu wa 2018.
 
4.Chelsea - Euro 190.9 milioni
Chelsea ililazimika kusajili kipya mpya wakati kwenye kikosi chao tayari kulikuwa na kipa mwingine wa kiwango cha dunia, Thibaut Courtois. Usajili huo wa kipa mpya, Kepa Arrizabalaga ulitokana na Courtois kulazimisha uhamisho wa kwenda kujiunga na miamba ya soka ya Hispania, Real Madrid. Kwenye hilo Chelsea hawakuwa na namna na hivyo kuweka rekodi kwa kumsajili kipa Kepa kwa mkwanja mrefu kutoka Athletic Bilbao. Walitumia pesa nyingine kuwanasa wachezaji kama Olivier Giroud, Emerson na Jorginho kwa mwaka huu wa 2018 na hivyo kukifanya kikosi hicho cha Stamford Bridge kuwa miongoni mwa timu zilizotumia pesa nyingi kwenye usajili mwaka huu, wakifanya manunuzi ya Euro 190.9 milioni.
 
3.Juventus - Euro 256.9 milioni
Juventus imetumia pesa nyingi sana kwenye dirisha la majira ya kiangazi, ambapo walitoa mkwanja mrefu kwenye usajili wa supastaa wa Ureno, Cristiano Ronaldo waliyemnasa kutoka Real Madrid. Kwenye usajili wa staa huyo, zaidi ya Euro 100 milioni zilitumika, kisha wakamnunua kumrudisha kwenye kikosi chao beki wa kati, Leonardo Bonucci. Waliwanunua jumla pia mastaa kama Douglas Costa na Joao Cancelo kuwaongeza kwenye kikosi chao na hivyo kuwafanya kutumia pesa nyingi sana kwenye dirisha hilo la majira ya kiangazi wakishika namba tatu katika timu iliyotumia mkwanja mrefu kwenye usajili kwa mwaka 2018, wakitumia Euro 256.9 milioni.
 
2.Liverpool - Euro 261.2 milioni
Liverpool ilifanya matumizi mazuri ya pesa waliyomuuza Philippe Coutinho kwa kumnasa beki wa kati Virgil van Dijk kwenye usajili wa dirisha la Januari na hivyo kumfanya Mdachi huyo kuwa beki ghali zaidi duniani. Kilipofika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya, kikosi hicho cha Anfield kinachonolewa na Mjerumani, Jurgen Klopp kilifanya usajili wa mastaa kibao wa maana, ikiwanaza Fabinho, Xherdan Shaqiri, Naby Keita na kipa Alisson Becker. Kutokana na hilo, Liverpool waliamua kufungua pochi ambapo uhamisho huo wa wachezaji umewafanya kutumia Euro 261.2 milioni kwa mwaka huu wa 2018 na sasa wanaoongoza ligi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…