Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu hawa hupaswa kulipwa kwa dola lakini baadhi ya makampuni wamekuwa wakiwalipa kwa Shilingi bila kuthaminisha fedha hiyo kutoka kwenye Dola za Marekani, hali ambayo husababisha wengi wao kulipwa fedha kiduchu ambazo hazikidhi.
 
Kama tujuavyo hapa nchini yapo makampuni zaidi ya 200 ambayo yanahudumia watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro na Mlima Meru, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba taarifa zilieleza kuwa kampuni ambazo zimekuwa zikiwahudumia vizuri wapagazi na waongoza watalii hazizidi tatu.
 
Taarifa hii ya kwamba kampuni za kuhudumia watalii zinazowahudumia vizuri kwa maana ya kuwalipa kwa kuzingatia misingi ya makubaliano wapagazi na waongoza watalii, hazizidi tatu na ni za kusikitisha kutokana na kwamba bila watu hawa, ni wazi kabisa kuwa utalii utazorota.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba watu hawa wanaoitwa waongoza watalii na wapagazi, wana umuhimu katika sekta ya utalii hasa tukiuzungumzia Mlima Kilimanjaro na Meru, kwa kuwa hawa ndio husaidia kuwaongoza watalii na kuwabebea mizigo yao hadi kumaliza utalii wao hapa nchini.
 
Back
Top Bottom