Jambo hili ni la kutazamwa kwa jicho la tofauti, kutokana na kwamba yapo madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kutokana na tatizo hili la wapagazi na waongoza watalii.
Moja ya mambo ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na tatizo hili ni baadhi ya wapagazi na waongoza watalii kutokuwa waaminifu na hata kijiingiza kwenye vitendo vya wizi ili kupata fedha za kujikimu wawapo mlimani na hata familia zao.
Tatizo la ukosefu wa uaminifu likizaliwa, linaweza kusababisha madhara makubwa katika sekta ya utalii, ikiwemo kuporomosha mapato yatokanayo na sekta hiyo kutokana na kwamba watalii wengi watahofia kufika nchini kwa ajili ya kupanda milima hiyo.
Jambo jingine ambalo linaweza kusababishwa na kuzaliwa kwa ukosefu wa uaminifu ni pamoja na kushuka kwa idadi ya watalii ambao wanafika nchini, kwa lengo la kupanda mlima Kilimanjaro na Meru na hivyo kuporomosha mapato yatokanayo na sekta ya utalii.
Ufike wakati sasa Serikali iliangalie suala hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu, ili kuweza kuiimarisha sekta ya utalii nchini na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa kupitia sekta hiyo.
Lakini lipo wazo ambalo limewahi kutolewa na Chama cha waongoza watalii la kuomba kuanzishwa kwa chombo kimoja kitakachowasimamia waongoza watalii na wapagazi, ni vyema Serikali ikalichambua wazo hili na kuona umuhimu wa kuunda chombo hicho
Chombo kama hiki kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko na ukandamizaji unaofanywa na kampuni zinazohudumia watalii nchini, kutokana na kwamba chombo hiki kitafuatilia kwa karibu na kuhakikisha wote wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria.
Pamoja na kuundwa kwake ni vyema sheria zikawepo na kubainisha wazi, kampuni zitakazokiuka mikataba na kuwalipa wapagazi kiwango kisichokidhi ni hatua zipi watakazochukuliwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.