Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20190102-WA0003.jpeg
 
Anaandika Benjamin James

Nyakati na Technology zimeharibu mambo mengi sana Tanzania.Wanawake wenye akili wasio na elimu walizaa na kulea ma Professors .

Nyakati hizi wanawake wasomi wanashindwa kuzalisha vizazi bora vya watoto wenye adabu,hekima na maarifa.

Nyakati hizi mwanamke jinsi anavyozidi kuelimika ndivyo anazidi kupoteza vinasaba maridhawa vya mke mwema na mama bora .

Uadirifu,unyenyekevu,lugha nzuri na majukumu ya mwanamke kwa mume imekuwa misimiati kwa asilimia kubwa kwa wanawake wasomi mwenye ndoa zao.

Mzazi anafurahia mtoto kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha,lakini mtoto hana adabu,ni mjeuri na mwenye kiburi,social media wazazi tunapost picture za watoto wetu kwa ubora wa mavazi na uzuri wa sura lakini hatujivunii haiba na tabia njema za watoto.

"She is my happines" mwingine utasikia "He is my handsome" lakini mtoto anamjua vyema house girl kuliko Mama.Wengi wamejificha kwenye kazi inachukua muda wangu mwingi nashindwa kukaa na mwanangu.

Wengine tumelelewa na wazazi ma -Nurse anaingia night lakini,tulisoma na kuimba table ya 1-12 ndio tulipewa ruhusa ya kwenda kucheza,tulifundishwa kufua na kupiga pasi na bado mzazi alikuwa busy na kazi.

Mtoto ni wa mama ,mama akikosa busara na hekima ya kulea watoto anaharibu kizazi chake,ukweli mchungu Tanzania divorce rate kubwa ni ya wanawake wasomi na wanaume wasomi,ndoa za watu ambao sio wasomi kuna ushirika na upendo mkubwa sana.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke mwenye akili asiye na elimu na mwanamke mwenye elimu asiye na hekima na busara.

Busara ina unyenyekevu,uvumilivu,adabu na utu, wanawake waliokosa busara utawagundua kwa show off na kauli zao.Jiulize mtoto wa kike wa miaka 8 anafuliwa chupi,anaandaliwa chai,kumiminiwa chain na anawekea sukari baba na mama wanaona ni haki.

Mtoto wa kike anasoma kidato cha nne anatumia IPhone 6 ,baba anatumia Techno ,mama anatumia Techno, mtoto anaongea na simu usiku kucha ,hakuna anayehoji simu kapata wapi,na pesa ya kununua airtime anapewa na nani?

Wazazi huwa wanahoji mimba ya nani na sio simu kakununulia nani?Mabinti wanapenda kusema,"Nataka mwanaume mrefu aliyejazia "baba yake mfupi na ana kitambi ,mama yako sio mjinga binti.

Wanaume wanapenda kuoa mwanamke mwenye kazi nzuri na elimu nzuri ,baba yako hakuwa mjinga kuoa mama yako darasa LA saba na kwenye ndoa miaka 40 na hakuna picture ya anniversary ya ndoa miaka 40 kwenye social media.

Vijana ambao hamjao wala kuolewa ,kigezo cha mke/mume mwema ni akili yake na sio elimu yake. Mungu humpa mtu kilicho bora.

Tujifunze kulea watoto kwa adabu,unyenyekevu na nidhamu na kukemea na kuadhibu kwa haki,tusijifiche mwenye kivuli cha kazi na ubusy.Binti anayefuliwa chupi miaka 10 anawezaje kuwa mke mwema?

Jiulize ni Mara ngapi umesali na mwanao kila aendapo shule? Ni Mara ngapi umeosha vyombo na binti yako? Ni Mara ngapi umemwambia mwanao baba/mama yako ni mtu bora kwangu na kwako?

[emoji2398]Benjamin James.
 
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Mwaka 1501-1504 Mchongaji maarufu wa sanamu wa kule italia Michelangelo alipewa kazi ya kuchonga sanamu ya Daudi na fa milia ya kitajiri ya nchini Italia katika mji wa Florence.

Kwa kuwa Michelangelo alikuwa maarufu kwa kazi hizo kitendo hicho kilivutia hisia za wengi kutaka kuona atakavyoichonga.

Kwa miaka miwili mizima alizunguka huku na kule akitafuta jiwe litakalofaa aina ya sanamu aliyotaka kuchonga. Siku moja pembeni mwa Barabara moja aliona jiwe lililokuwa limeotewa na magugu na lilikuwa na uchafu. Alipolikwangua kidogo akagundua ni jiwe aina ya Mable.

Akawaagiza vijana wake waliviringishe hadi kwenye karakana yake. Akatumia miaka miwili kulipiga nyundo na kuchonga ili kupata picha rough ya Daudi.

Kisha akatumia miaka miwili tena kulipiga msasa na kusawazisha vizuri ili kupata sanamu kamili. Yenye urefu wa mita 5 na nchi17

Kazi ilipomalizika sanamu ile ilipelekwa kwenye Town square ( uwanda wa mji ) wa Florence ili kuzinduliwa.
Mara ilipofunguliwa watu waliokuwa wametoka kila pembe ya Italia kuja kuangalia sanamu hii walipigwa na butwaa na baadhi ya wanawake walizimia kwa ustadi iliochongwa na uzuri wake.

Baadaye walipomuuliza Michelangelo amewezaje kuchonga sanamu nzuri vile jibu lake lilinishangaza. Akasema
"Mimi nilimuona Daudi akiwa amekamilika ndani ya lile jiwe, kazi yangu ilikuwa ni kuondoa kile ambacho sio Daudi."

Leo unaweza ukawa ni Daudi ambaye umejificha ndani ya magugu ya mashaka, hofu, uvivu, na kutokujiamini.

Mwaka 2019 uutumie kuondoa kile ambacho sio we we ili ubaki wewe. Ndani yako Mungu ameweka MTU mkubwa sana lakini bado hujamwona. Kuna vipaji ambavyo vimefunikwa na uchafu. Kazi yako ni kuuondoa ili Daudi aonekane.

Mafunzo kutoka kwa Michelangelo.

1. Alimuona Daudi ndani ya jiwe akiwa amekamilika. Leo jione ukiwa umekamilika na mwenye uwezo wa kufanya chochote kile.

2: Tumia muda mrefu kujinoa, soma vitabu, tafuta maarifa ya vile unavyotaka kuwa baadaye. Yeye alitumia miaka 6 hadi kukamilisha kazi.

3; Fanya mambo kwa ubora. Michelangelo angeweza kutumia vijiwe vidogo kuchonga sanamu lakini alitumia miaka 2 kutafuta jiwe tu hadi akapata lililokuwa bora zaidi.

4: Fikiria impact utakayoacha duniani baada ya wewe kuondoka. Leo ni miaka 515 imepita lakini limejengwa jumba la makumbusho mjini Florence kuilinda sanamu hiyo isiharibike na inaendelea kuingizia pesa za utalii nchi ya Italia kwa watu wanaoenda kuitembelea.

Kumbuka mwaka huu ondoa kile ambacho sio wewe ili ubaki wewe.

The best way to learn is to learn from the best. happy new year
 
*Mambo mazuri tushirikishane*

INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA

FEES SCHEDULE 2018-2019 SCHOOL YEAR

Early childhood 1-2 - USD 17,300= *38,060,000/-*

Kindergarten - grade 5 - USD 19,200= *42,240,000/-*

Grades 6-8- USD 22,300 = *49,060,000/-*

Grades 9&10- USD 23,700= *52,140,000/-*

Grades 11&12-USD 28,600= *62,920,000/-*

APPLY NOW

P.O BOX 2651,
DSM
255 22 2152350
 
*HOW TO LOCATE YOUR WIFE IN A CROWD WITHOUT WASTING YOUR AIRTIME CREDIT*

If you go to a function, and there are many people. suddenly, your wife went to greet her friend, from there you can't locate her again, don't stress yourself calling her, just look for another beautiful lady and start talking to her, before you ask of her name your wife will be standing next to you.....

Its another way of saving your phone credit...wisdom will kill me..I'm I lying?[emoji41]
 
*Mambo mazuri tushirikishane*

INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA

FEES SCHEDULE 2018-2019 SCHOOL YEAR

Early childhood 1-2 - USD 17,300= *38,060,000/-*

Kindergarten - grade 5 - USD 19,200= *42,240,000/-*

Grades 6-8- USD 22,300 = *49,060,000/-*

Grades 9&10- USD 23,700= *52,140,000/-*

Grades 11&12-USD 28,600= *62,920,000/-*

APPLY NOW

P.O BOX 2651,
DSM
255 22 2152350
[emoji16][emoji16][emoji16] hata nikitumia kikokotoo kipya(25%) bado napata tabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom