Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Emery amefahamishwa kwamba Arsenal hawataunga mkono mpango wake wa kutaka kuwarejesha Calum Chambers, 23, na Reiss Nelson, 19, mwezi huu. Wawili hao wako nje kwa mkopo. (Metro)
 
Chelsea wanakariiba sana kukamilisha usajili wa kiungo wa kati Mmarekani Christian Pulisic, 20, kwa £45m kutoka Borussia Dortmund. (Express)
 
Monaco wanapanga kukamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas, 31, mwezi huu wa Januari, hatua ambayo itamkutanisha na mchezaji mwenzake wa zamani Arsenal Thierry Henry ambaye sasa ni meneja. (Daily Mail)
 
Mkufunzi mkuu wa Chelsea Maurizio Sarri amesisitiza kwamba hahitaji kununua mshambuliaji mwingine Januari hata kama jeraha la kifundo cha mguu linalomtatiza Olivier Giroud litazidi. (ESPN
 
West Ham wanapanga kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Everton James McCarthy, 28, kama sehemu ya mpango wao wa kuimarisha kikosi chao Januari. (Daily Mail)
 
Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, hataki kuitwa arejee katika klabu hiyo kwa sababu anafurahia maisha yake kwa Aston Villa kwa mkopo, anasema meneja Dean Smith. (Sky Sports
 
Klabu ya Chelsea imemsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau la Yuro 64m lakini itamtoa kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwisho wa msimu,
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Marekani , ambaye alikuwa amehusishwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal , alijiunga na Dortumund akiwa mchezaji mchanga 2015.
Pulisic amefunga magoli tisa katika mechi 23 akiichezea Marekani.
''Ilikuwa ndoto ya Christian kujunga na ligi ya Uingereza'' , alisema mkurugenzi wa klabu ya Dortmund Michaek Zorc.
 
Hiyo ni kutokana na mizizi yake ya Marekani na kutokana na hilo tulishindwa kuongeza mkataba wake.
''Na sasa tumekubali ombi zuri la Chelsea''.
Kandarasi ya Pulisic katika klabu ya Dortmund ilitarajiwa kukamilika kufikia 2020.
Katika taarifa iliojaa hisia aliyochapisha katika mtandao wake wa Twitter, Pulisic alisema kuwa anaondoka Dortmund 'shingo upande'.
''Nahisi kama jana wakati nilipowasili katika klabu ya Dortmund, nikifurahia wakati nilipokuwa na umri wa miaka 16 kutoka mji mmoja mdogo wa Hershey nchini Marekani'', alisema.
 
''Nisingalikuwepo hapa bila ya klabu hii na imani yao ya kuwapatia fursa wachezaji wachanga''.
''Kwa miezi sita ijayo, ni Dortmund pekee. tafadhalini musiwe na wasiwasi kuhusu upendo wangu , bidii na asilimia 110 ya kuichezea timu hii hadi nitakapopiga mpira wa mwisho msimu huu''.
 
Ni mmoja ya wachezaji wachanga wanaosakwa Ulaya'
Pulisic alianza kuichezea klabu hiyo ya Bundelsiga akiwa na umri wa miaka 17 mnamo mwezi Januari 2016 na miezi miwili baadaye aliitwa kuichezea timu yake ya taifa.
Amecheza mechi 81 katika ligi kuu ya Ujerumani na mechi 20 katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Amefunga magoli matatu katika mechi 18 katika mashindano yote msimu huu akiichezea Dortmund.
 
Mkurugenzi mkuu wa Chelsea Marina Granovskai alimtaja Pulisic kuwa miongoni mwa wachezaji bora wanaotafutwa Ulaya.
''Akiwa na umri wa miaka 20 , tunaamini ana uwezo kuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa miaka mingi ijayo'', alisema.
Mchezaji huyo ndio wa kwanza kusajiliwa na Chelsea tangu dirisha la uhamisho lifunguliwe tarehe mosi mwezi Januari.
 
Ni mchezaji wa tatu anayelipwa pesa nyingi katika ligi ya Bundesliga, baada ya Ousmane Dembele aliyehamia Barcelona kutoka Dortmund kwa dau la £135m mwaka 2017 na dau la £55m alilonunuliwa Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg mwaka 2015.
Chelsea wako katika nafasi ya 4 katika ligi ya Premia, alama 11 nyuma ya Liverpool.
Dortmund inaongoza katika jedwali la ligi ya Bundesliga kwa pointi sita na atakabiliana na Tottenham katika awamu ya mechi za kuingia robo fainali.
 
Yaani Bongo mtu ukitaka kuchapisha kitabu ni lazima uombe ruhusa siku hizi? Hiyo ruhusa unaomba kwa nani? Na hao TRA wanahusikaje? Kama haya mambo yapo basi we can't be siriazi...
Kitabu kitapatiwa kodi za kutosha bado gharama za uchapishaji,kama gazeti tukuchapishwa lina mlolongo sembuse kitabu,ingekua rahisi tungekua na vitabu vya kutosha mitaani hadi mitandaon kwa lugha ya kiswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…