Hongera kwa wachezaji hawa wazuri ajabu. Hivi ndivyo tunahitajika kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Timu zote mbili zilijaribu kushambulia, hatukuwa na wasiwasi, hatukuwa na woga, na tulikuwa na presha sana.
"Wao ni viongozi, ni alama nne lakini tumepunguza mwanya. Tulifahamu kwamba tungeshinda mechi hiyo tungekuwa na nafasi ya kushindania ubingwa Ligi ya Premia, tukishindwa basi ndoto kwisha.
"Sikumbuki ni ligi ligi ilikuwa ngumu hivi, kuna klabu nyingi kubwa zinazoshindania taji. Kila mechi ni kama fainali."