Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Safari hii Man United imetangaza vita kuwa italipa pesa inayotakiwa na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ili kumnasa Pochettino, lakini Spurs imekuwa akiweka ngumu kwa sababu inataka ihamie kwenye uwanja wake mpya ikiwa na kocha bora kabisa kwenye benchi lake. Kocha mwingine, anayehusishwa na kibarua hicho jina lake likitajwa sana ni Zinedine Zidane.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid CV yake iko vizuri na jambo zuri kwa sasa hana kazi, hivyo kumpata kwake huhitaji kutoa pesa kama ilivyo kwa Pochettino.
 
Laurent Blanc, aliyewahi kuichezea Man United naye yupo kwenye orodha hiyo. Awali kocha huyo alitakiwa kupewa kibarua cha muda wakati Mourinho alipofutwa kazi, lakini jina lake liliwekwa kando na Solskjaer akapewa kazi hiyo. Hata hivyo, Blanc yupo kwenye orodha ya wanawania kibarua cha kudumu cha kuinoa Man United.
 
Man United imeripotiwa pia kwenye majina hayo ya makocha wanaotaka kazi huko Old Trafford, yupo pia Julian Nagelsmann wa Hoffenheim.
Ni kocha kijana na hilo linaonyesha msimamo wa mabosi hao wa Man United katika kujenga timu ya kizazi kipya. Nagelsmann ni kocha wa kizazi kipya, mwenye mbinu za kisasa anayechuana na wakali kama Jurgen Klopp, Pochettino na wengineo akiwamo Pep Guardiola.
 
Man United imeripotiwa pia kwenye majina hayo ya makocha wanaotaka kazi huko Old Trafford, yupo pia Julian Nagelsmann wa Hoffenheim.
Ni kocha kijana na hilo linaonyesha msimamo wa mabosi hao wa Man United katika kujenga timu ya kizazi kipya. Nagelsmann ni kocha wa kizazi kipya, mwenye mbinu za kisasa anayechuana na wakali kama Jurgen Klopp, Pochettino na wengineo akiwamo Pep Guardiola.
 
Jina la mwisho kabisa kwenye orodha hiyo ya makocha ndilo lililoshangaza wengi. Kuna kocha anaitwa Marco Rose. Kocha huyo wa Salzburg ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kuifanya timu ndogo ya Austria kuwa tishio kwenye Europa League msimu uliopita, kocha huyo aliifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali. Alishinda pia ubingwa wa ligi na anaonekana kulirudia hilo msimu huu.
 
Jurgen Klopp anaamini nahodha wa Manchester City Vincent Kompany alifaa kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ambayo Liverpool walilazwa 2-1 uwanjani Etihad.

Kompany alionyeshwa tu kadi ya manjano kwa kumchezea visivyo mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah dakika ya 32.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji alimkaba Mo Salah kwa kuruka miguu yake yote ikiwa hewani kana kwamba anateleza. Alimgonga Salah kwenye kifundo chake cha mguu.

Leroy Sane alifunga bao la ushindi dakika ya 72 na kupunguza uongozi wa Liverpool hadi alama nne.
 
Kompany aliondolewa uwanjani dakika ya 88 na nafasi yake akaingia Nicolas Otamendi.

"Nampenda sana Vincent Kompany lakini inakuwaje kwamba hiyo si kadi nyekundu?" Klopp alishangaa baada ya mechi.

"Ndiye mtu wa mwisho safu ya ulinzi anapomkabili. Akamgonga Mo vyema, basi hataweza kucheza tena msimu huu. Sio rahisi kwa mwamuzi na huenda hakuona nilivyoona mimi."

Kompany alitofautiana na tathmini ya Klopp kuhusu tukio hilo lililotokea mambo yakiwa 0-0.
 
Nilifikiri nilikaba vyema, sivyo? Niliupata mpira, na kiasi kidogo nikampata yeye. Lakini hakukuwa na nia mbaya," Mbelgiji huyo alisema.

"Sikumuumiza. Ilikuwa ni nimkabili au nimwache aende akafunge."

Klopp alisema ni kweli timu yake haikucheza vyema sana lakini kwa kiasi fulani bahati haikusimama.
 
Matarajio yetu yalikuwa makubwa. Tunaweza kucheza vyema zaidi. Ni lazima uichukulie mechi ilivyo. Hauwezi kutawala wakati wote," aliongeza.

"Kulikuwa na presha sana. Ilikuwa mechi kali na ya kasi. Tulikosa bahati nyakati muhimu za kutaka kufunga bao. Tulikosa bahati zaidi ya City, ninaweza kusema hivyo.
 
Back
Top Bottom