Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutokana na hilo, ndio maana imeweka orodha ya washambuliaji wengi inayowataka akiwamo Edinson Cavani na Gonzalo Higuain. Washambuliaji hao wakitua Stamford Bridge, basi watawasahaulisha mashabiki wa The Blues shida za washambuliaji wao wa sasa, Alvaro Morata na Olivier Giroud ambao wamekuwa butu kuliko neno butu lenyewe. Kwenye dirisha hili la Januari, mashabiki wa Chelsea watafarijika sana kama watafanikiwa kuinasa moja kati ya saini za wachezaji hao, hasa Higuain, ambaye ni rahisi kumpata na pia amekuwa akifahamiana vyema na Kocha Maurizio Sarri kwa sababu walishawahi kufanya kazi pamoja huko kwenye kikosi cha Napoli.
 
Lakini shida kubwa inayoikabili haina mshambuliaji wa kusaidiana na Kane na Mwingereza huyo anapokuwa majeruhi, basi shida inakuwa kubwa kwenye kikosi hicho cha Kocha Mauricio Pochettino. Kutokana na hilo, Spurs inahitaji huduma ya mshambuliaji matata kabisa wa Kibrazili kama vile Richarlison, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kabisa huko katika kikosi cha Everton.
 
2.Man City - Sergio Busquets

Manchester City ni moja kati ya timu zenye vikosi bora kabisa duniani, lakini shida ni moja inahitaji mtu mwingine kwenye sehemu ya kiungo wa kukaba kwa sababu Fernandinho umri unazidi kumtupa mkono. Ni kitu ambacho hakina kificho kiungo huyo wa Kibrazili hawezi kuendelea kucheza hadi kwenye umri wa miaka 40. Kutokana na hilo, Man City inahitaji huduma ya mtu matata kabisa kama kiungo wa Kihispaniola, Sergio Busquets. Usajili wa staa huyo wa Barcelona ukifanyika utakuwa umemfurahisha kila mtu na sasa Man City itakuwa haikamatiki kwenye sehemu yake ya katikati ya uwanja.
 
Lakini itakuwa moto na tamu zaidi kama itainasa huduma ya kiungo fundi wa mpira wa Kihispaniola, Isco. Staa huyo kwa sasa mambo yake sio mazuri huko Real Madrid kwenye kikosi cha Kocha Santiago Solari, hivyo itakuwa usajili matata utakaomfurahisha kila shabiki wa Liverpool kama atanaswa na kutua Anfield kwenye dirisha la Januari. Kwa namna Liverpool ilivyoteswa na viungo wa Man City kwenye mechi iliyopita, inahitaji kuwa na huduma ya mbunifu kama Isco.
 
42364921-d941-4f89-a2b2-a8f8d4a6437c.jpeg
 
Lakini itakuwa moto na tamu zaidi kama itainasa huduma ya kiungo fundi wa mpira wa Kihispaniola, Isco. Staa huyo kwa sasa mambo yake sio mazuri huko Real Madrid kwenye kikosi cha Kocha Santiago Solari, hivyo itakuwa usajili matata utakaomfurahisha kila shabiki wa Liverpool kama atanaswa na kutua Anfield kwenye dirisha la Januari. Kwa namna Liverpool ilivyoteswa na viungo wa Man City kwenye mechi iliyopita, inahitaji kuwa na huduma ya mbunifu kama Isco.
 
SUPA Sergio. Wanamwita hivyo, ukiweka kando ile a.k.a yake ya utotoni Sergio ‘Kun’ Aguero. Kwa kifupi tu ni bonge la straika linalobamba huko kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England akitupia jezi za wababe wa Etihad, Manchester City.
 
Alhamisi iliyopita uwanjani Etihad, Aguero alipiga bonge la bao wakati kikosi chake cha Man City kilipoichapa Liverpool 2-1 na kuzirudisha mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England kuwa tena na upinzani mkali.
 
Mastaa wanaomfuatia kwa kufunga mabao mengi kwenye mechi zilizohusisha timu za Big Six tangu msimu wa 2011-12 ni straika Harry Kane, amefunga mabao 21, Wayne Rooney amefunga mabao 20, Robin van Persie amefunga mabao 18 na supastaa wa Chelsea, Eden Hazard amefunga mabao 17.
 
Aguero pia amekuwa kiboko ya Liverpool wanapokwenda kucheza kwenye Uwanja wa Etihad. Fowadi huyo amefunga katika mechi zote saba alizoichezea Man City dhidi ya Liverpool kwenye mechi ya Ligi Kuu England uwanjani Etihad.
 
Back
Top Bottom