Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama inazuumika acha tuendelee kuizuumu...
Ezi ifu kashika parachichi
IMG_20190109_160410.jpeg
 
Chelsea inatarajiwa kuanza mazungumzo na mshambuliaji nguli wa AC Milan, Gonzalo Higuain ikitaka saini yake Januari, mwakani.

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amevutiwa na kiwango bora cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina katika kufunga mabao.

Higuain aliwahi kunolewa na Sarri katika msimu wa mwaka 2015-2016 alipokuwa kocha wa Napoli ya Italia.

Taarifa ya Sarri imekuja saa chache baada ya Chelsea kulala bao dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Kombe la FA uliochezwa juzi usiku.

Mshambuliaji huyo anacheza kwa mkopo AC Milan akitokea kwa ‘Kibibi Kizee’ cha Turin, Juventus.

Hata hivyo, Higuain mwenye miaka 31 amefunga mabao manane katika mechi 20 alizocheza AC Milan yenye maskani San Siro.
 
Mshambuliaji wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah ametangazwa mchezaji bora wa Afrika 2018.

Salah ametwaa tuzo hiyo katika hafla iliyohudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo Rais wa Liberia George Weah.

Mshambuliaji huyo amepata mafanikio hayo baada ya kufunga mabao 32 ya Ligi Kuu England na 44 katika mashindano yote msimu 2017/2018.
 
Nyota huyo alifunga mabao mawili katika fainali za Kombe la Dunia ambazo Misri ilishiriki kwa mara ya kwanza, baada ya kupita miaka 28.

Pia nahodha huyo wa Misri mwenye miaka 26, aliisaidia Liverpool kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei, mwaka jana.

Salah aliibuka kinara katika hafla iliyofanyika juzi usiku mjini Dakar, Senegal ambapo alimpiku mchezaji mwenzake Sadio Mane na nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.
 
Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Salah aliyetwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, alipanda jukwaani na kucheza muziki.

Salah alipata kura nyingi zilizopigwa na wakurugenzi wa benchi la ufundi na makocha kutoka nchi 56, mwanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kikosi bora Afrika kinaundwa na Salah, Mane, Aubemeyang, Naby Keita, Riyad Mahrez, Eric Bailly , Serge Aurier, Medhi Benatia, Kalidou Koulibaly, Thomas Partey na kipa Denis Onyango.
 
Sir Alex Ferguson amewaeleza wachezaji wa Manchester United watarudisha hadhi ya klabu hiyo kama ilivyokuwa enzi zake.

Pia Ferguson amesema atampa kila aina ya ushirikiano kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer, katika kampeni yake ya kuisuka upya Man United.

Kauli ya kocha huyo wa zamani wa timu hiyo mwenye historia ya pekee, imekuja muda mfupi baada ya Solskjaer kushinda mechi tano mfululizo dhidi ya Cardiff City, Huddersfield, Bournemouth, Newcastle United na Reading.
 
Nguli huyo alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa timu hiyo ana nafasi ya kurudisha hadhi ya Man United katika ramani ya soka kwa kuwa ana wachezaji bora.

Ferguson amewataka wachezaji kuipigania Man United katika mechi zote za mashindano kwa kuwa wana uwezo na viwango bora vya kucheza soka.

Kocha huyo alitoa kauli hiyo alipoalikwa na Solskjaer kwenda uwanjani kuzungumza na wachezaji ikiwemo kuwajengea uwezo wa kujiamini katika mechi za mashindano.
 
Back
Top Bottom