Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Taarifa za kutoka Ufaransa zinadai wenyeji wa fainali zijazo za Kombe la Dunia wanamtaka kocha huyo akanoe kikosi chao kutokana na uzoefu wake kwenye mchezo wa soka.

Huko nyuma, kabla ya kuibuka kwa dili hilo, Wenger alikuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kuwa mkurugenzi wa michezo kwenye kikosi cha PSG, lakini sasa anaweza kwenda kukamatia kazi hiyo ambayo italipa zaidi.
 
Wenger siku zote amekuwa na ndoto za kwenda kuwa kocha wa timu ya taifa na pengine sasa huo unaweza kuwa wakati mwafaka kwake katika kutimiza ndoto hiyo ya muda mrefu.

Umri wake wa sasa ni miaka 69, hivyo inatazamwa pia kama atakuwa na uwezo wa kunoa timu katika fainali hizo za Kombe la Dunia 2022.

Kocha Wenger alisema pia anavutiwa na usajili unaofanywa na Kocha Unai Emery, ambaye ametua huko Emirates kuchukua mikoba yake. Emery amesajili wachezaji kadhaa akiwamo kiungo Lucas Torreira anayefanya vizuri kwa sasa.
 
WASHAMBULIAJI watatu matata kabisa wanaoishika Ligi Kuu England kwa sasa, Mohamed Salah, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang wamechaguliwa kuunda safu ya ushambuliaji ya kikosi cha kwanza cha mwaka cha wachezaji wa Afrika.
 
Mo Salah, anayekipiga kwenye kikosi cha Liverpool ameshinda pia tuzo ya kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka wa pili mfululizo, hivyo kwenye kikosi hicho cha Afrika atajumuika na staa mwenzake wa Anfield, Mane pamoja na fowadi matata wa Arsenal, Aubameyang.
 
Lakini kikosi hicho cha mwaka cha Afrika ni kama kimejaa wanasoka wa kutoka kwenye Ligi Kuu England, ambapo wengine walionaswa ni Serge Aurier, Eric Bailly, Naby Keita na Riyad Mahrez, ambao watafiti kwenye mfumo wa 4-3-3.
 
Salah alifunga mabao 44 kwenye kikosi cha Liverpool na Misri mwaka 2018, huku akishinda pia Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England msimu uliopita.
 
Mane yeye alifunga mabao 20 katika mechi 44, wakati msimu huu hadi sasa ameshafunga mabao tisa katika mechi 26. Aubameyang ni kinara wa mabao huko Arsenal, akifunga mara 16 katika mechi 26, wakati msimu uliopita alifunga mabao 10 katika mechi 13 alizoichezea Arsenal baada ya kujiunga nayo akitokea Borussia Dortmund, Januari 2018.
 
Aurier, anakipiga kwenye kikosi cha Tottenham naye ameingia kwenye kikosi hicho, huku Eric Bailly wa Manchester United, Riyad Mahrez wa Manchester City na Naby Keita nao wakiwamo kwenye orodha.
 
Beki wa Napoli, anayewindwa na Man United, Kalidou Koulibaly, naye amepata nafasi sawa na Medhi Benatia wa AS Roma, huku kipa wao ni Denis Onyango wa Uganda.
 
Kocha huyo amewataka wachezaji kujenga utamaduni mpya wa kutaka ushindi katika mechi zote ambazo Man United itacheza dhidi ya wapinzani.
 
Kocha huyo wa muda alisema kuwa ana timu imara ya ushindi ambayo ina nafasi ya kufanya vyema endapo wachezaji watajituma.
 
Solskjaer, mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, alisema ana amini atajifunza mengi kupitia mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs.
 
Nimebaini kuna muunganiko mzuri wa pamoja. Kimsingi hali ni nzuri, timu imara. Tuna mechi moja au mbili ngumu hilo ni deni,” alisema kocha huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…