Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kujitolea ni kuamua kufanya jambo kwa jamii si kwa kutegemea faida japo faida tena kubwa yaweza kujitokeza baadaye. Kwa mfano, kijana anapohitimu masomo yake anakuwa hana uzoefu na kazi nyingi katika matangazo yake yanahitaji mtu awe na uzoefu wa miaka kadhaa katika taaluma yake, unadhani uzoefu utapatikana wapi wakati kila mwenye kazi anahitaji uwe na uzoefu?
 
Inasemekana kuwa chanzo cha watanzania kutokuwa na moyo wa kujitolea ni ukoloni uliomuathiri mtanzania kisaikolojia. Ikumbukwe kuwa watanzania walikuwa wakilazimishwa kufanya kazi katika mashamba na maeneo mengine ya kazi zao suala ambalo liliwaumiza sana watanzania kwa kitendo hicho na ndio chanzo cha kupeana POLE kwa kazi. Moyo wa kupenda kazi bila malipo ulikufa na ndio maana ukimkuta mtu anafanya kazi unamwambia POLE KWA KAZI…
 
kiuhalisia unadhani nani apewe pole kati ya mwenye kazi na asiye na kazi? Ni jambo la kawaida kusikia kuwa mtu hana kazi na ametafuta kazi kwa muda mrefu hajapata na wengine wanakata tama ya maisha kwani kila siku ni kuzunguka huku na huku kutafuta kazi lakini hawapati. Labda kwanza tuone maana ya kazi kwani yawezekana tusiwe tunajua;
 
KAZI NI NINI?
Nijuavyo mimi, kazi ni shughuli yoyote iliyo halali au isiyo halali yenye manufaa kwako au kwa jamii.
ANGALIZO: Ukifanya kazi isiyo halali katika nchi yenye sheria iliyo kinyume na kazi hiyo… unaweza kuchukuliwa hatua. Mfano, kwa Tanzania ukifanya kazi ya kuuza bangi itakuwa haramu na ukikamatwa utajibu katika vyombo vya sheria na yawezekana ukafia jela.
 
Kutokana na maelezo hapo juu, kumbe kazi sio zile za kuajiriwa tu bali hata za kujiajiri pia ni kazi ili mradi tu ziwe na manufaa kwako au kwa jamii.
Kutokana na utamaduni wa kutojitolea tuliojipandikizia tangu enzi zile, kwa watanzania walio wengi, ukisema unaomba nafasi ya kujitolea kufanya jambo fulani hawakuamini maana wamezoea ule msemo kuwa no free lunch in London… wanajua una lako jambo maana sio moyo wa mtanzania.
 
Sasa, kutokana na hali hii..watanzania tutaendelea kuwa maskini kwani mwenye nacho hawezi kumpatia mwingine BURE kwani wanadhani ni MTEGO na watalipishwa tu. Mi sioni kama kuna haja ya kuendelea kukumbatia mawazo haya kwani naona kama yanarudisha maendeleo nyuma, fikiria, mtu ukimnyima nafasi hata ya kujitolea, uzoefu ataupata wapi?
 
Hebu angalia wasomi wengi walivyojaa mtaani na bado hali ya nchi ni tete katika Nyanja zote, kwanini wasitumiwe walau kuongeza ubora wa hali?
Lakini pia tuangalie na kwa upande wao je, wana moyo wa kujitolea? Wengine wanadhani kujitolea lazima katika taasisi au kampuni fulani ili nawe uonekane kama muajiriwa wa sehemu fulani, angalia mazingira uliyomo, anzia hapo hapo…mfano, umesomea masuala ya mazingira, kwanini mtaani kwako hapaeleweki?
 
Hebu angalia wasomi wengi walivyojaa mtaani na bado hali ya nchi ni tete katika Nyanja zote, kwanini wasitumiwe walau kuongeza ubora wa hali?
Lakini pia tuangalie na kwa upande wao je, wana moyo wa kujitolea? Wengine wanadhani kujitolea lazima katika taasisi au kampuni fulani ili nawe uonekane kama muajiriwa wa sehemu fulani, angalia mazingira uliyomo, anzia hapo hapo…mfano, umesomea masuala ya mazingira, kwanini mtaani kwako hapaeleweki?
 
Mazingira ni machafu hadi nzi wanashangilia, cha kushangaza nawe upo na unazidi kutafuta ajira mwaka wa nne sasa na unasubiri wakuajiri ndo ufanye mazingira yale kuwa salaama! Tatizo laweza kuwa ulichokisomea hukijui…..kama umesomea masuala ya mazingira, mbona yako yamekushinda?
 
Ninaposema hivi nina ushahidi wa kutosha..nimeshuhudia miradi mingi ikianzishwa baada ya mtu kuanza kimchezo mchezo na vishughuli vidogo vidogo vya kijamii na baada ya mchango wake kuonekana mbunge wake kwa ujanja wa kisiasa akatoa support, habari zikamfikia waziri husika, akmuunganisha na wafadhiri, na sasa ni mradi mkubwa sana.
Wanaposema mtu aajiajiri hawamaanishi uanzishe biashara yoyote na kuacha fani uliyosomea, unaweza kujiajiri kwa kupitia fani hiyo hiyo na kuweza kufikia malengo uliyojipangia.
 
Kuna wanaosema kozi walizosomea ni mbaya hazina fursa za kujiajiri, inawezekana…lakini ulisomaje kozi ambayo hukuifanyia utafiti, na yawezekana pia hukuwa na malengo katika maisha na kupelekea kusoma kwa kufuata mkumbo.
 
USIJILAUMU, badili mtazamo na anza kuwa mbunifu, anza na kero unayoiweza iliyopo mtaani kwenu, jaribu kuitatua kwa uwezo wako mdogo, na MUNGU atakusaidia upate mafanikio kwani kama hutapata support, basi bidii yako ikishaonekana wenye nafasi za ajira watakutafuta na kukuomba wakuajiri bila kutuma maombi wala interview.
 
KILA TOKEO LINALOKUTOKEA linakuwa na chanzo ambapo tokeo hilo laweza kuwa zuri au baya. Siku zote tunafanya mambo bila kujua kama yana manufaa kwetu au la! Na wakati mwingine tunajali faida tuzipatazo sasa na kujifanya hatujui kama tunatakiwa kuandaa maisha ya baadae pia.
 
UAMUZI ndio unaokupatia tokeo sahihi au baya. Kuna watu wasioamua bali husubiri wengine wawaamulie, hilo ni kosa kubwa sana katika maisha ya mwanadamu kwani maisha ni yako na wewe ndio mhusika mkuu katika igizo la wewe kuishi. Wengi tunaigiza katika maisha na ndio maana nayaita maisha kuwa ni maigizo. Ishi maisha yako na uukatae umaskini.

AMUA VYEMA, UPATE MATOKEO MAZURI, na kila tokeo linatokana na uamuzi.
 
Back
Top Bottom