Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Marcos Rojo na Fred hawakuonekana kwenye kambi hiyo na wenzao, wakati wakijifua kwenye viwanja vya Nad Al Sheba Sports Complex.

Alipoulizwa Kocha Solskjaer kuhusu mastaa hao alisema: “Marcos Rojo amerudi nyumbani kwa sababu ya majeraha yake kuwa makubwa tofauti na ilivyofikiriwa. Fred anatarajia mtoto.”
 
Kwenye kikosi cha kwanza, mastaa hao wawili Rojo na Fred ndio wanaompunguzia hesabu Kocha Solskjaer katika mkakati wake wa kuwapa mambo matamu wachezaji wake wote, huku akiwambia ni afya kwa wachezaji wa timu moja kulumbana ndani ya uwanja kama ikionekana mmoja hatimizi majukumu yake ipasavyo.Kuondoka kwa Jose Mourinho, maisha ya wachezaji yameonekana kuwa na furaha zaidi kwa sasa.
 
.NI hivi Arsene Wenger anaweza kubamba dili jipya la kazi baada ya Qatar kumweka kwenye orodha ya kumtaka awe kocha wao mkuu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022.

Kocha huyo Mfaransa kwa sasa yupo tu akisubiri kazi mpya baada ya kupigwa chini na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kudumu na timu hiyo kwa miaka 22.
 
Taarifa za kutoka Ufaransa zinadai wenyeji wa fainali zijazo za Kombe la Dunia wanamtaka kocha huyo akanoe kikosi chao kutokana na uzoefu wake kwenye mchezo wa soka.

Huko nyuma, kabla ya kuibuka kwa dili hilo, Wenger alikuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kuwa mkurugenzi wa michezo kwenye kikosi cha PSG, lakini sasa anaweza kwenda kukamatia kazi hiyo ambayo italipa zaidi.
 
Wenger siku zote amekuwa na ndoto za kwenda kuwa kocha wa timu ya taifa na pengine sasa huo unaweza kuwa wakati mwafaka kwake katika kutimiza ndoto hiyo ya muda mrefu.

Umri wake wa sasa ni miaka 69, hivyo inatazamwa pia kama atakuwa na uwezo wa kunoa timu katika fainali hizo za Kombe la Dunia 2022.
 
thee_sonia_3___BrSTz0fF-n4___.jpg
 
LAZIMA kieleweka na kitaeleweka tu. Kocha, Unai Emery amepata mzuka huko Arsenal baada ya mastaa wake kibao waliokuwa wagonjwa kupona na sasa wapinzani imekula kwao. Hapo kati, Arsenal ilikuwa na udhaifu mkubwa kutokana na mastaa wake kadhaa muhimu kuwa majeruhi, lakini kwa taarifa tu kuna vifaa sita matata vimerejea mazoezi na kukifanya kikosi cha wababe hao wa Emirates sasa kuwa kamilikamili katika mchakamchaka wao wa kuhakikisha kwamba suala la kumaliza msimu ndani ya Top Four haliwi tena mjadala mzito.
 
Kocha, Emery alikuwa kwenye wakati mgumu sana kwenye mechi zilizochezwa hapo kati kutokana na kukosa huduma za wachezaji wake muhimu, lakini sasa mambo yamekaa sawa na West Ham United ndio watakaoanza kukutana na Arsenal iliyokamilika kwenye idara zake.
 
Wachezaji sita muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal walikuwa wakikosekana kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa wagonjwa, lakini sasa mambo yatakuwa tofauti kuanzia na kwenye mechi zijazo. Mesut Ozil na Hector Bellerin ni miongoni mwa mastaa hao sita waliokuwa hawapo kwenye kikosi cha Arsenal kwa kuwa majeruhi, lakini sasa watarudi uwanjani na sura zao zitaonekana kwenye mechi ya wikiendi hii dhidi ya West Ham. Ozil amekosekana uwanjani tangu alipotolewa uwanjani wakati wa mampumziko kwenye mechi dhidi ya Brighton kwenye Boxing Day kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
 
Lakini, Mjerumani huyo sasa yupo fiti na amerudi mazoezini huku akiwa na kazi moja ya kumshawishi kocha Emery ili akipige wakati wababe hao watakapomenyana na West Ham kesho Jumamosi. Bellerin mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Desemba 6 kwenye mechi ya kipigo dhini ya Southampton. Kurejea kwa mchezaji huyo kunatazamiwa kwenda kupunguza presha kwenye safu ya mabeki ya timu hiyo ambayo siku za karibuni imekuwa ikiruhusu mabao kuliko maelezo.
 
Mastaa wengine wanne wanaoungana na wawili hao ambao wanarejea kwa kishindo kwenye chama la Arsenal ni Laurent Koscielny, Shkodran Mustafi, Nacho Monreal na Dinos Mavropanos, ambao wanakuja kumfanya Emery sasa kutibu yale matatizo yaliyokuwa yakisumbua kwenye kikosi chake, kuwa na beki mchekea. Koscielny aliumia wakati akipasha misuli moto kabla ya mechi ya Blackpool, wakati Mustafi alikosa mechi hiyo kwa kuwa na tatizo la misuli. Monreal naye alikosa mechi kibao mwezi uliopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.
 
Back
Top Bottom