Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Cengiz Under

Manchester United wameripotiwa kuungana na wapinzani wake kwenye Ligi Kuu England, Arsenal na Tottenham Hotspur katika mbio za kumfukuzia winga wa AS Roma, Cengiz Under. Staa huyo bado ana mkataba mrefu huko Stadio Olympico ambao utafika kikomo 2022, hivyo mkwanja ambao utapaswa kutumika kumwondoa kwenye kikosi hicho cha Serie A unapaswa kuwa mrefu kwelikweli. Kutokana na kocha Solskjaer kuanza vyema kibarua chake cha muda huko Man United mabosi wa timu hiyo hawatakuwa wamekosea kama atatumia pesa kusajili mchezaji mpya kabla ya dirisha hili la Januari kufungwa ili kukipa nguvu kikosi hicho cha Old Trafford.
 
WAYNE Rooney amempongeza Ole Gunnar Solskjaer, lakini amewaambia mabosi wa Manchester United wasiache kumwaajiri Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mpya kwa msimu ujao.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Man United, Rooney alisema kocha Pochettino ndiye mtu anayeifaa zaidi timu hiyo licha ya Solskjaer kufanya vyema kwa sasa. Rooney anakoshwa na utaratibu wa Pochettino wa kuwapa wachezaji makinda nafasi na kukuza viwango vyao.
 
Rooney amesema kwamba Solskjaer anastahili kupewa nafasi ya kuwa kocha wa kudumu kwenye kikosi hicho baada ya kubadili hali ya kikosi ndani ya muda mfupi aliotua Old Trafford kama kocha wa muda kuchukua mikoba ya Jose Mourinho.
Rooney alisema: "Kitu cha kwanza unapaswa kumpa nafasi Ole kwenye mjadala wa kocha wa kudumu na baada ya hapo, basi mtu mwingine wa kufanya naye majadilianno ya kibarua hicho basi awe Pochettino.
 
Nadhani Manchester United - kwa miaka zaidi ya 20 au 30 tangu walipokuwa chini ya Alex Ferguson - wamekuwa wakitegemea wachezaji makinda inaowazalisha wenyewe. Mimi nadhani Pochettino nni bora zaidi kwenye matumizi ya wachezaji vijana. Hebu tazama wachezaji vijana aliowaibua huko Tottenham na Southampton wote wamepata nafasi ya kucheza kwenye timu ya taifa.
"Hilo lina maana kubwa sana unnapokuwa kocha kwa Pochettino yupo na utayari kwenye kuwapa nafasi wachezaji vijana."
 
Rooney amekiri kwamba kwa sasa Man United imeanza tena kuvutia kuitazama baada ya kuwa timu ya hovyo kwa kipindi kilichopita hasa walipokuwa chini ya Mourinho ambaye mara nyingi Mreno huyo alikuwa bize kulumbana na wachezaji wake.
 
Solskjaer alisema hakuna kitu kinachowatia presha Liverpool na Man City kwa sasa zaidi ya kasi ya Man United kwenye ligi hiyo, hivyo amewaambia wachezaji wake kwa sasa piga ua wameshindwa mengina, basi ni lazima wachukue nafasi ya tatu.
 
Man United hawapo kwenye mbio za ubingwa, lakini anaamini wakipambana na kushika namba tatu ndani ya siku chache zijazo, basi jambo hilo litawafanya Liverpool na Man City kupata ugonjwa wa kutetemeka.
 
49368314_583788968759193_5211404844365039469_n.jpg
 
Ole amekuwa na uhakika wa timu yake kuwamo kwenye nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, baada ya Jumapili iliyopita kushinda kwenye uwanja mgumu wa Wembley dhidi ya wagumu Tottenham Hospurs.
 
Solskjaer alisema: “Nataka wachezaji wangu kujiamini, watulize daluga zao uwanjani kwa sababu hilo ndilo jambo muhimu zaidi na kubwa kwangu.”

Ushindi dhidi ya Spurs uliwafanya Man United kuwafikia kipointi Arsenal na kuwa pointi sita nyuma ya timu inayoshika namba nne Chelsea, lakini sasa matokeo ya jana yatakuwa yameleta kitu tofauti kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kwa namna anavyoisimamia timu hiyo kwa sasa, Ole amepewa nafasi ya kuwa kocha wa kudumu mbele ya Mauricio Pochettino, ambaye pia ana nafasi kubwa ya kuchukua kibarua hicho baada ya Jose Mourinho kutupiwa virago vyake mwezi uliopita.
 
Solskjaer alisema: “Kila mtu alisema Tottenham ulikuwa mtihani mzito kwetu. Sikuona hilo jaribio, kwa sababu wachezaji walikuwa tayari kwa ajili ya mechi yoyote ile.

“Sasa tunasubiri kucheza nyumbani na timu zinazoonekana tunaweza kuzimudu. Hizo ni nafasi za kupanda juu kwenye msimamo wa ligi. Kama tukicheza kila mechi kama wanavyopaswa, nina uhakika kuna kitu kikubwa kitawashtua wapinzani wetu.”

Ole alikuwa matata akiwa mchezaji kwenye kikosi hicho cha Old Trafford kabla ya sasa kuja kutengeneza mizizi yake akiwa kwenye benchi la ufundi.

Kuona kwamba Ole hana shida na Man United, ndio maana kwa sasa anatafuta makazi ili aondoke hotelini, Lowry. Mourinho aliishi kwenye hoteli hiyo kwa muda wake wote wa miaka miwili na nusu aliyodumu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

“Bado nipo hotelini, lakini natafuta makazi. Nimetembezwa huko mtaani kutafuta nyuma inayofaa kuishi.”
 
Watu kote duniani wanatarajiwa kuona kupatwa kwa mwezi utakaobadilika na kuwa mwekundu .
Wakati wa kupatwa kwa mwez,i dunia hutoa kivuli chekundu.
Kupatwa huko kwa mwezi kutaonekana kutoka kaskazini na Kusini mwa Marekani pamoja na maeneo ya magharibi mwa Ulaya ikiwemo Uingereza na kaskazini mwa Afrika.
 
Kupatwa kwa mwezi ni nini?
Tukio hili hujiri wakati dunia inapopita katikati ya Jua na mwezi.
Katika hali hii, jua huwa nyuma ya dunia huku mwezi ukizunguka katika kivuli cha dunia.
Je mwezi mwekundu ni upi?
 
Back
Top Bottom