Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

49519963_114497469618467_6219814043137475380_n.jpg
 
Yaruhusu magumu yapite, hatuwezi kuyatatua yote sawa mamaangu. Mambo mengine yanaisha kwa kuyaweka wazi kwa mtu wako aliye jirani, unao majirani wengi sana humu, niwe mkweli wanasaidia sana. Ongea na Pyaar, ongea na Shimba, ongea na Myoya, ongea na Yego, ongea na carba, ongea na..... Wapo wengi sana.
Mimi usijaribu, maana bado lile somo la mlonge sijalifanyia majaribio,natafuta konokono....
Hahahahahahaa anko bana
 
Kocha huyo aliyewahi kuwa mshambuliaji wa timu hiyo huko nyuma jana Jumamosi aliongoza Man United kwenye mechi yake ya saba, wakifukuzia ushindi ili kuweka rekodi tamu kabisa baada ya kushinda nyingine zote zilizopita. Hiyo jana, Man United walitarajia kucheza na Brighton uwanjani Old Trafford.
 
Kikosi cha Man United kwa sasa kinacheza vizuri tangu walipomwondoa kocha Jose Mourinho, lakini hilo halina maana kwamba hawahitaji kufannya marekebisho kwenye kikosi hicho ili kuwa makini zaidi ndani ya uwanja. Kutokana na hilo suala la kufanya usajili halipingiki na ndio maana kumeorodheshwa majina ya mastaa kadhaa ambao ambao bila shaka watatua kwennye kikosi hicho cha Old Trafford kama si kwenye kipindi hiki cha dirisha la usajili wa Januari basi lile la baadaye litakalofanyika mwishoni mwa msimu.
 
Kalidou Koulibaly

Kalidou Koulibaly wa Napoli ameshajitengenezea jina na kumfanya atambulike kwamba mmoja wa mabeki wa kati bora kabisa duniani kwa sasa. Ubora wake ndani ya uwanja ndicho kitu kinachomfanya staa huyo wa Senegal kuwa kwenye rada za klabu nyingi kubwa za Ulaya. Si jambo lenye kificho kwamba Koulibaly atakwenda kuifanya beki ya Manchester United kuwa imara zaidi kama atafanikiwa kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha hili la Januari au lile likalo la mwisho wa msimu ili kuwafanya kama Virgil Van Dijk alivyobadili upepo huko Liverpool. Taarifa za kutoka Italia zinafichua kwamba kama Man United watapeleka ofa rasmi ya kumtaka beki huyo basi Koulibaly mwenyewe ataandika barua ya kuwaomba Napoli wamuuze.
 
Philippe Coutinho

Mashabiki wa Liverpool watakuwa wanapiga sana sala kuona jambo la kiungo wa Kibrazili, Philippe Coutinho kuhamia Manchester United halitimiii. Hata hivyo, hizo zitabaki kuwa sala tu hazitaendana na ukweli hali kama imepangwa kutokea, itatokea tu. Coutinho alinaswa kwa pesa nyingi sana na Barcelona, Januari mwaka jana wakati wababe hao wa Nou Camp walipotoa zaidi ya Pauni 140 milioni kupata huduma ya mchezaji huyo kutokea Liverpool. Lakini, huko na huko mambo yamekuwa magumu na Barca wanaripotiwa kwamba wapo tayari kusikiliza ofa inayomhusu Coutinho na hapo Mann United wakaanzna kuhusishwa. Inaelezwa kwamba mke wa Coutinho hataki kurudi England kwa sasa kutokana na kwamba ametoka kujifungua mtoto wa kike, lakini kwa jambo hilo basi usajili huo unaweza kufanyika mwisho wa msimu.
 
David Brooks

Tottenham Hotspur wameripotiwa kuingia kwenye vita dhidi ya Manchester United kwa ajili ya kumnasa staa wa Bournemouth, David Brooks. Mchezaji huyo ameibukia kwa kasi kwenye Ligi Kuu England na kubamba kinoma tangu alipotua Bournemouth akitokea Sheffield United Julai mwaka jana. Kiwango chake cha msimu huu kimekuwa juu sana na kuwavutia timu nyingi vigogo wanaopambana kuhakikisha wananasa saini yake. Staa huyo wa kimataifa wa Wales amefunga mabao matano msimu huu na umri wake bado mdogo, miaka 21 tu, hivyo amekuwa na wakati mzuri mbele yake wa kukua na kuwa mchezaji bora kabisa mchezo huo wa soka kama atapewa nafasi ya kucheza kila wakati.
 
Nikola Milenkovic

Beki huyo wa Fiorentina kwa muda mrefu sana amekuwa kwenye rada za Manchester United wakidaiwa kuhitaji huduma yake huko Old Trafford.

Bila ya shaka, Man United ipaswa kufungua pochi yake kupata saini ya beki huyo wa kati wa kimataifa wa Serbia, huku ikifahamika wazi kwamba anaweza kupatikana katika dirisha hili la usajili wa Januari. Nikola Milenkovic anaweza kucheza kwenye beki ya kati au beki ya kulia na umri wake ndio kwanza miaka 21 hivyo bado ana wakati mzuri zaidi wa kukuza kiwango chake na kuwa mchezaji bora kabisa kwa simu za baadaye kama Man United itafanikiwa kuinasa huduma yake.
 
Back
Top Bottom