Solskjaer alisema: “Kila mtu alisema Tottenham ulikuwa mtihani mzito kwetu. Sikuona hilo jaribio, kwa sababu wachezaji walikuwa tayari kwa ajili ya mechi yoyote ile.
“Sasa tunasubiri kucheza nyumbani na timu zinazoonekana tunaweza kuzimudu. Hizo ni nafasi za kupanda juu kwenye msimamo wa ligi. Kama tukicheza kila mechi kama wanavyopaswa, nina uhakika kuna kitu kikubwa kitawashtua wapinzani wetu.”
Ole alikuwa matata akiwa mchezaji kwenye kikosi hicho cha Old Trafford kabla ya sasa kuja kutengeneza mizizi yake akiwa kwenye benchi la ufundi.
Kuona kwamba Ole hana shida na Man United, ndio maana kwa sasa anatafuta makazi ili aondoke hotelini, Lowry. Mourinho aliishi kwenye hoteli hiyo kwa muda wake wote wa miaka miwili na nusu aliyodumu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
“Bado nipo hotelini, lakini natafuta makazi. Nimetembezwa huko mtaani kutafuta nyuma inayofaa kuishi.”